Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Books
  • Publish
  • Sell
  • Courses
  • Blog
  • Support
  • Sign in

Recent Posts

  • Download vitabu 21 vya mahusiano na ndoa
    25 Sep, 2026
  • Book review: ZAKA: Hukumu, Faida na Hekima Zake
    22 Sep, 2026
  • Mfahamu Mwandishi: Khalifa L. Simion - Mwandishi anayeigusa jamii ya Kiislamu
    10 Sep, 2026
  • Mfahamu Mwandishi: Daudi Lubeleje - Mwandishi nyuma ya vitabu 14
    5 Sep, 2026
  • Vitabu 25+ vya Biashara, Fedha na Uchumi
    27 Aug, 2026
  • Book review: Amazing Animal Coloring Book for Kids
    11 Jul, 2026
  • Mapitio ya kitabu: Utambulisho Wako Katika Kristo
    21 Jun, 2026

Categories

  • Book Recommendations
  • Book Reviews
  • Help & Support
  • Offers and discounts
  • Reading Habits & Tips
  • Writing, Publishing & Author Support
  • Author Spotlight

Start selling your book or course on our website — reach more readers

You will enjoy high book visibility, get paid on time and receive a monthly sales report straight to your inbox.

Start selling →

Kama mwandishi wa vitabu unataka kufanikiwa kwenye nini?

March 9, 2022 at 7:38 pm,


Chapisho hili tumelitoa katika blogi ya Daudipages

Kuna utafiti nilishiriki hivi majuzi wa Belinda K Griffin kutoka SmartAuthorsLab.com ambao ulitaka kujua, wewe kama mwandishi unataka kufanikiwa kwenye nini? Ulikuwa ni kuchagua moja kati ya majibu haya;


  1. Kupiga pesa
  2. Kufikia wasomaji wengi zaidi na ujue vitabu vyako vinapendwa
  3. Kupata michongo ya biashara
  4. Kujulikana tu kama nawe ni mwandishi au mtaalamu kwenye eneo unaloandika
  5. Kushinda tuzo za uandishi

Jibu nililotoa katika utafiti huu ni siri yangu, vipi wewe ungechagua lipi hapo?. Kilichonifanya niandike chapisho hili ni kwamba, Belinda ameshea nami matokeo ya awali ya utafiti huu na yamekuwa ni matokeo ya kushangaza kidogo. Hebu tuone,

  • Kuwafikia wasomaji wengi na kujua kwamba wana furahia na kuvipenda vitabu vyako ndiyo jambo kubwa ambalo waandishi wengi wanataka. Utafiti unasema 83.8% ya waandishi walisema wanapenda tu vitabu vyao vifike kwa wasomaji kuliko kupiga pesa na kunufaika na waandishi wao ambayo ilipata 2.7% tu. Je! Kwa sababu waandishi wengi hawataki kupiga pesa kwenye uandishi wao (2.7% tu ya waandishi walisema ndo wanataka), itakuwa ndiyo sababu waandishi wengi hawana pesa ijapokuwa vitabu vyao ni vizuri na watu wanapenda?, au Je! Inawezekana waandishi wanaweka juhudi kidogo sana kwenye kuuza vitabu vyao na wanabaki kufurahia tu kuona kitabu kinapendwa?.
  • 86.5% ya waandishi hawarudishi gharama zao za kuandaa vitabu vyao. Pengine hii inaweza sababisha na dhana kwamba, wao wanapenda tu kuona vitabu vinapendwa na wasomaji lakini si kupiga pesa. Lakini jambo la kusikitisha zaidi, 68.4% ya waandishi walisema wao wanajua jinsi ya kufikia malengo yao ijapokuwa nachelea kusema isijekuwa ni ndoto za abunuasi.

Get a Free PDF

Enter your email to get a free PDF "Hatua 6 rahisi za kuandika kitabu"

Thank you!

Go to your email inbox to download your free PDF

.

Niseme tu kwamba, mimi binafsi nimekuwa nikiwasaidia watu wengi kuwa waandishi waliofanikiwa kwa kuwapa ushauri wa bure, kuandika makala kama hii na mwaka jana mwishoni nilianza kuandaa kozi za kuwasaidia waandishi zaidi. Sasa ikiwa ungetaka usaidizi wangu ili ufanikiwe kwenye uandishi wako na usiwe miongoni mwa 83.8% ya waandishi ambao wana vitabu vizuri lakini hawana pesa, chukua hatua sasa kwa;

  • Weka miadi ya kuongea na mimi hapa bure
  • Anza kusoma kozi sasa hivi hapa
  • Ji subscribe kupata Makala kama hii kwenye baruapepe yako hapa

Karibu kuweka comment yako hapa chini.



Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Books
  • About us
  • Publish
  • Sell
  • Blog
  • Support
  • Sign in
DL Bookstore © 2026. All rights reserved | Made with ❤️ in Tanzania.