Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support

Unapata changamoto kuuza kitabu chako?

April 27, 2022 at 7:40 pm,


Hata kama haisemwi na waandishi wengi, lakini ukweli unabaki kuwa waandishi wanaugulia maumivu ya ndani kwa ndani wanapoona vitabu vyao haviuzi.

Mimi pia, kama mwandishi, naelewa ninachosema. Wakati natoa kitabu changu cha kwanza, nilikuwa na matarajio kuwa, ndani ya miezi michache tu, nakala 500 ambazo nilikuwa nimetoa zingeisha haraka sana, halafu nitoe nyingine zaidi. Lakini haikuwa hivyo. Hata hivyo sikukata tamaa.


Nataka kukwambia hata wewe ambaye unapata changamoto ya kutokuuza nakala kwamba usikate tamaa. Unaweza kunishangaa, “hivi Daudi unajua anachoongea?”, ndio! Nina sababu kukwambia hivyo.

Nina habari njema!, Nimepata suluhisho la kumsaidia mwandishi kuuza nakala nyingi. Baada ya uzoefu wa miaka kadhaa katika kuuza vitabu na kujaribu mbinu na njia mbalimbali za kuuza vitabu jumlisha uzoefu wa waandishi wengine ambao wamenishirikisha, nimekuandalia kozi ya siku 8 inayoitwa Sanaa ya Uuzaji wa Vitabu. Lengo la kuandaa kozi hii ni moja tu, kukusaidia wewe kuuza nakala nyingi, sitaki ukwamishwe na changamoto ya kutouza mpaka unakata tamaa.

Ndani ya kozi hii kuna nini?

Kozi hii ya siku 8 ina jumla ya mada 7 ambazo utakuwa unapata mada moja kila siku, zoezi kila mwishoni mwa mada ya siku, na mtihani mmoja ambao utakuwa siku ya mwisho ya kozi (siku ya nane). Ukishamaliza, nitakupatia cheti cha kukupongeza na kuhitimisha kozi.

Je! Hizo mada 7 ni zipi;

  • Mada ya kwanza: Mtazamo sahihi kuhusu uuzaji wa vitabu
  • Mada ya pili: Kuweka mkakati wa kuuza kitabu
  • Mada ya tatu: Mbinu ya Bullseye Framework (BF)
  • Mada ya nne: Unahitaji nini ili ufanikiwe?
  • Mada ya tano: Ujuzi wa kutoa kitabu bure kimkakati
  • Mada ya sita: Uchaguzi wa njia za kuwafikia wasomaji wako
  • Mada ya saba: Jinsi ya kujenga jukwaa lako kama mwandishi

Baada ya kumaliza kozi hii na ukafanyia kazi mbinu na njia ambazo utajifunza, changamoto ya kutouza kitabu itakuwa umeishinda.

Kozi inaanza lini?

Kwanza kabisa, kozi ni self-paced yaani unasoma kwa muda wako utakaochagua uwe unapokea mada. Kozi itakuwa hewani kwa wote wanaotaka kuanza kusoma siku ya Jumamosi 30/04/2022 mapema kabisa asubuhi. Nifafanue kidogo hapa, haimaanishi kwamba usipoanza Jumamosi, basi utakuwa umechelewa, hapana ila siku ya Jumamosi ndiyo itakuwa hewani kwa mara ya kwanza, baada ya hapo anayetaka kusoma ataikuta ipo tu inamsubiri.

Kozi ni automated, kwa mfano, siku ya Jumamosi nikaanza kuisoma mida ya saa tatu kamili asubuhi, basi kwa siku zote zilizosalia, nitapokea mada muda huo huo wa saa tatu kamili asubuhi.

Kozi itafundishwaje?

Utoaji wa kozi ni kupitia baruapepe yako, kwa hiyo mada zote, kwenye muda ule ule ulioanza kusoma siku ya kwanza, utapokea mada kwenye baruapepe yako utakayotumia kuisoma kozi hii. Kwa hiyo utahitaji kuwa na baruapepe, halafu, nywila yake nitakupatia

Kuna gharama yoyote jamani?

Gharama ipo, ila nimeamua kuupiga mwingi kuanzia leo mpaka siku ya Jumamosi, nimetoa OFA kwa wote watakaojisajili kabla ya kuanza kozi, unalipia elfu 10 tu! Halafu kuanzia Jumapili gharama itapanda mpaka elfu 20!.

Unasubiri nini sasa? Jisajili sasa hivi

USAJILI WA KOZI

Weka jina lako, namba ya simu na barua pepe yako, kisha bonyeza TUMA TAARIFA pale mwishoni mwa fomu hii.

N.B: KOZI ITAANZA 30/04/2022

Gharama ya kozi

Kozi nzima itagharimu kiasi cha 20000/= LAKINI LIPIA KWA OFA 9999/= tu! kukamilisha usajili wako.

N.B: Fanya malipo kwenda 0764771298 au 0621460465 [Jina ni Daudi Lubeleje]. Kama ukitaka kutuma kwenda bank bonyeza HAPA

.

Kuna kozi nyingine hivi?

Ndio! Kozi zingine zilizopo ni

  1. Jinsi ya kuandika na kutoa eBook
  2. Mwongozo wa kuzindua kitabu kwamafanikio

Ahsante!

Karibu kwa maoni, maswali na mapendekezo hapa chini.

Credit: Chapisho hili tumelitoa katika blogi ya DaudiPages 



Recent Posts

  • Mambo 10 ya Kujifunza Kutoka Kitabu cha Hamasika Kila Siku
    29 Jun, 2025
  • Download Vitabu 7 vya Fedha (PDF)
    19 Jun, 2025
  • Kutoka Daftari Hadi Kitabu Halisi: Jinsi ya Kugeuza Maandishi Yako Kuwa Kitabu
    16 May, 2025
  • Umechoka na Minyama Uzembe? Suluhisho la Kupungua Uzito Limepatikana!
    17 Apr, 2025
  • Vitabu Bora vya Pasaka vya Kukuimarisha Kiroho – Vinapatikana Sasa DL Bookstore
    11 Apr, 2025
  • 4 Benefits of Selling Your Book Through DL Bookstore
    20 Mar, 2025
  • Download Entrepreneurship Books (PDF) in Swahili
    10 Feb, 2025

selling_book-1.png

Enroll in 100% free courses

100% free courses on writing, publishing, and marketing of books. Time to dive in!

Start learning →

Cart

Cart is empty.

Log in




Forgot password?
Create account
Login to existing account
My orders
My reviews
My details
Log out
  • Home
  • Get books
  • About us
  • Author services
  • Blog
  • Support
  • Client portal
DL Bookstore © 2018 - 2025. All rights reserved.