Fanya mambo haya 3 uuze sana kitabu chako
Ndoto ya kila mwandishi anapoandika kitabu ni kuuza nakala za kutosha. Kitabu chako kinapoingia sokoni unafanya kila unaloweza kiuze na kama hakiuzi lazima ujiulize kwanini. Sasa tujiulize, mafanikio ya mwandishi kwenye kuuza kitabu chake huchangiwa na nini?
Kuna mambo 3 ambayo ukiyafanya lazima kitabu chako kitaua nakala za kutosha, mambo hayo ni haya;
1. Toa kitabu bora. Kuna msemo husemwa kwamba ni msomaji ambaye husema hiki kitabu ni bora. Lakini, wewe kama mwandishi lazima uhakikishe kitabu chako kinatoka bora kuanzia ndani mpaka nje. Hakikisha mchapishaji wako anakitoa kitabu vizuri sana. Huwa inanoga pale msomaji anaposhika kitabu chako, anasema huyu mwandishi alikuwa makini na kazi yake na aliwekeza vya kutosha kupata kazi bora. Inapotokea kitabu chako kimetoka vibaya, msomaji hupata picha ya haraka umelipua lipua hata kama umeandika maudhui bora sana. Jambo la kwanza unapotaka kitabu chako kiuze, fanya kila unaloweza kitabu kitoke vizuri.
Unataka kujua zaidi kuhusu uandishi wa vitabu? Soma kozi bure HAPA na kuwa wa kwanza kupata taarifa za kozi mpya kila inapowekwa.
2. Lielewe soko lako vema unalolenga. Ukweli
mchungu ambao waandishi wengi huwa hawaukubali ni kuwa kitabu chako
hakitapendwa. Kuelewa soko lako ni kuelewa ni wasomaji wa aina gani
ulowaandikia. Kitabu chako kinafaa kwa kundi lipi?. Ili ujue soko lako la
kitabu litakuwa kwa wasomaji gani unaweza kutumia njia hizi kukusaidia kujua
kwa haraka
a. Anza na kuwaangalia waandishi wanaoandika aina ya kitabu kama chako. Mfano, kama unaandika riwaya, angalia waandishi wengine wanaoandika riwaya kama wewe. Kama wasomaji fulani wanapenda vitabu vya DaudiPages basi bila shaka watapenda na vyangu kwa sababu zipo kundi moja.
b. Angalia wasomaji wako wanapatikana wapi zaidi. Si wasomaji wote wako Facebook ama kwa makundi ya WhatsApp, unaweza kuta wasomaji wako ni wale wanaopenda kwenda kununua vitabu kwa maduka ya vitabu. Ukishajua wasomaji wako wanapatikana wapi zaidi, basi hakikisha unawawekea kitabu chako huko ili wakipate kwa urahisi.
3. Jalada la kitabu liendane na aina ya kitabu
ulichoandika. Fikiria umeandika riwaya lakini jalada la kitabu linaonekana kama
kitabu cha biashara vile, haitakupa matokeo mazuri sokoni. Ukitaka kuuza nakla
nyingi za kutosha, jalada la kitabu chako ni silaha bora ya kuwanasa wasomaji
wako.
Karibu kwa comments hapa chini.