Kuandika kitabu inahitaji jambo moja tu.
Huwa inaonekana kama kuandika kitabu inataka ufanye mambo mengi sana ambayo, kwa wanaoingia kwenye uandishi kwa mara ya kwanza, huonekana yanachanganya mno. Habari mbaya ni kuwa, wengine hukata tamaa wanapoona mchakato kuwa mgumu, lakini leo nataka kuamsha ndoyo yako ya kuandika kitabu inayotaka kufa.
Nikwambie tu kwamba kuandika kitabu inataka ufanye jambo moja tu, nalo ni hili, fikiria kuandika kitabu kama mchakato unaohusisha mambo matatu, mambo hayo ni yapi?
Wazo la kuandika. Ili mambo yawe rahisi sana, tumia aplikesheni kama vile Evernote, Zoho notebook na nyingine nyingi ambazo unaweka tu kwenye simu kutoka Playstore ya Google. Kwanini aplikesheni hizi? Zinakusaidia kuandika na kuhifadhi kila wazo jipya unalopata la kuandika. Unapata mawazo mengi lakini kama huna mahali utaandika basi utasahau, na kila unaposahau unaona kuandika kitabu ni kazi ngumu, kumbe sivyo.
Mswada wako. Yale mawazo yote uliyopata ukayaandika na kuyahifadhi kwenye aplikesheni yako kama nilivyokueleza hapo juu ni wakati sasa wa kuandaa miswada yake. Unachomoa wazo moja, unatulia na kuandika. Kama unapata changamoto ya kukosa muda wa kuandika, chapisho hili Unaupataje muda wa kuandika kitabu? Litakusaidia sana.
Uhariri wa miswada yako. Hili ndilo jambo la mwisho, mswada wako unahaririwa na kazi inakuwa imeisha. Nafikiri sasa umeona jinsi ilivyo rahisi kuandika kitabu ukifanya mambo haya matatu kwa mtiririko huu, zingatia tu kutokuruka hatua.
Kwa ufupi tu, kusanya mawazo yako unayopata, usiache yapite hivi hivi, pengine hilo wazo ulilonalo sasa ndiyo kitabu chako kitakachouza sana. Halafu, andika miswada yako na fanya uhariri bila haraka wala presha. Nini kinafuata baada ya uhariri? Tuwasiliane kwa ushauri zaidi, bofya hapa.
Karibu kwa comments hapa chini.