[Mpya] Soma vitabu hivi ufuge kuku kitalaamu
Maarifa ya ufugaji wa kuku, sasa yapo karibu na wewe kuliko hapo awali tena kwa gharama nafuu tofauti na kama ungeenda chuo kusoma kwa miaka mingi. Mtalaamu wa ufugaji wa kuku, Mr. Mujaya Jones Mujaya ameandika vitabu hivi viwili ambavyo ukivisoma vitakupa hamasa ya wewe kupiga hatua ya kuanza ufugaji wa kuku kitaalamu.
Baada ya kukamilisha uandaaji wa vitabu hivi, yaani kusanifu majalada yake na ubunifu wa kupangalia kurasa za ndani, tuliongea na Mr. Mujaya Jones Mujaya atuandalie maelezo mafupi kuhusu vitabu vyake ili upate, kwa ufupi tu, kile kimeandikwa ndani ya vitabu hivi.
1. UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI KAMA MRADI - “Hatua kwa Hatua Kuelekea Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji Wenye Faida”
Kwenye kaya nyingi mijini na vijijini kuna kuku wa kienyeji wanaofugwa. Sehemu kubwa kila baada ya nyumba 3 hadi 5 kwenye mtaa basi moja inafuga hawa kuku.
Licha ya kufugwa kwa wingi, bado bei ya mazao yake yani kuku, nyama, mayai na vifaranga bado ipo juu sana ukilinganisha na aina nyingine za kuku. Kuku wa kienyeji ni kitoweo kinachopendwa sana. Bado hakuna sherehe ya maana bila nyama ya kuku wa kienyeji.
Pamoja na manufaa haya na kuuzwa bei nzuri sokoni bado watu hawanufaiki na kuku huyu. Kuku wengi wanapotea kwa vifo, magonjwa, ajali, wizi, kushambuliwa wanyama au wadudu wakali na kupotea. Wafugaji wanaojinasibu kufuga kuku hawa kwa wingi wengi wana idadi ya kuku chini ya mia moja (100).
Changamoto kubwa inayosababisha hali hii ni ufugaji wa mazoea usiozingatia mbinu za kitaalamu pamoja na kibiashara. Kuku wanatelekezwa bila kupatiwa huduma za msingi kwa sababu mfugaji hana elimu au taarifa sahihi hivyo anashindwa kufanya maamuzi sahihi anapopatwa na majanga kama vile magonjwa ya mlipuko.
Ili pawepo na tija, ufugaji wa kuku wa kienyeji unapaswa kuendeshwa kitaalamu kwa kuzingatia kanuni bora za ufugaji kama mradi wa biashara. Lazima upate faida kwenye kila pesa unayotumia kwenye kufuga kuku.
Kitabu cha "Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji Kama Mradi" ni mbia wako muhimu kukupatia ujuzi wa mbinu hatua kwa hatua kuelekea ufugaji wa kuku wa kienyeji wenye faida.
Kitabu kinakupatia hatua zilizothibitika za kufanya uanze kuona manufaa kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji. Utajua hatua unazotakiwa kupita kuanzia kwenye wazo la kufuga hadi utakapofika sokoni. Utapata ufahamu wa kudhibiti magonjwa na gharama za chakula cha kuku.
Ndani ya kitabu kuna mbinu za kuzalisha kuku wengi na mazao yao kwa gharama nafuu sana hivyo hautapata kisingizio cha kutoona faida kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji. Utaweza kuanza kufuga vyoyote utakavyo bila hofu ya mtaji.
Kitabu hiki nimekitohoa kwenye makala yangu maarufu ya "Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji Kama Mradi" ambayo imewanufaisha maelfu ya watu ndani na nje ya Tanzania wanaoelewa lugha ya kiswahili.
Baadhi ya shuhuda zao hizi hapa:
Likaa Likaa
“Sijapata kuona elimu bora ya ujasiriamali kama hii. Safi sana yani safi. Elimu mliyotoa ni njema na Mungu awabariki. Kwa mtu makini na mfuatiliaji hii ndiyo investment bwana. Safi! Big Up!”
Laurensia Mallya
“Asante sana mtoa darasa kwani nimepata uelewa mkubwa kutokana na makosa niliyokuwa nayafanya bila kufahamu sasa nitazingatia elimu yako uliyonipa.”
Joseph Masenta
“Asante sana mtoa darasa, ninaamini sasa katika ajira kama hizi kwa mwaka unaweza kupata mamilioni ya pesa.”
Jimmy James
“Asante! Nimejifunza kitu, nilikuwa nikitafuta jinsi ya ufugaji wa kuku wa kienyeji sasa nimepata darasa tosha.”
Victor Ezekiel Kamaghe
“Asante sana kwa elimu yako nzuri. Mie bado sijafanikiwa kuuanzisha mradi ila kupitia darasa hili lazima nitafanya.”
Daniel Mkongwa
“Nimependezewa sana sana na mradi huu, naanza na kuku 30 nataka nione matokeo yake, naamini Mungu ataniongoza.”
2. ONGEZA KIPATO CHAKO NA KUKU WA KIENYEJI - “Mbinu Rahisi na Haraka za Kufuga Kisasa na Kitaalamu kwa Mfugaji Anayeanza Biashara.”
Tunaishi katika kipindi ambacho bei za bidhaa zinapanda sana wakati thamani ya fedha inazidi kushuka. Kila kukicha watu wanapata hofu ya uwezo wao wa kuendelea kumudu mahitaji ya kila siku.
Utaona hata uwezo wa watu kupata mahitaji ya lazima ya maisha kama vile chakula, mavazi na makazi au malazi umepungua. Ajira zimekuwa changamoto kupatikana na zikipatikana kipato chake kinakuwa kidogo sana ambapo ni vigumu kuona unafuu wa maisha.
Hakuna mitaji. Mabenki, wafadhili, wadhamini na taasisi za kifedha zinaangalia sana usalama wa fedha zao hivyo ni vigumu kuwakopesha wajasiriamali wanaoanza.
Kutokana na changamoto hizi kuna mahitaji makubwa ya mbinu za kujikwamua katika hali hiyo. Huenda tayari hadi unaposoma hapa umejaribu njia nyingi za kujikomboa bila mafanikio.
Jamii inahitaji suluhisho rahisi kwa changamoto za ajira na hali duni ya maisha. Suluhisho ambalo litamkwamua mtu ndani ya muda mfupi bila kutumia rasilimali nyingi na ambalo litamfaa kila mtu bila kujali umri wake kwenye mazingira yote.
Suluhisho hilo ni Ufugaji wa kuku wa kienyeji. Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni fursa kubwa ya kuongeza kipato chako na familia yako. Kila mtu kwenye kaya anaweza kunufaika kupitia mradi huu.
Ni fursa ambayo kuanzia mtoto anayesoma shule ya msingi ya kutwa au bweni hadi mtu mzee kabisa yani kikongwe anaweza kuichangamkia. Ni fursa mtambuka kwani pamoja na kuboresha chakula cha familia moja kwa moja pia inaongeza kipato cha kaya.
Kitabu cha "Ongeza Kipato Chako na Kuku wa Kienyeji" kitakupatia mbinu rahisi za haraka na kitaalamu za kufuga kuku wa kienyeji hata kama ndiyo unaanza. Lengo ni kukusaidia unayeanza ufugaji huu uufanye kiurahisi lakini upate mazao mengi kwa muda mfupi zaidi.
Kwa mfugaji wa kuku wa kienyeji kitabu hiki kitakupa mbinu za kuboresha ufugaji wako uanze kupata faida endelevu. Utaweza kupanua mradi wako uwe shughuli rasmi ya kiuchumi siyo kupata mboga ya kukarimu wageni au kama kitoweo cha sherehe na sikukuu tu.
Hiki ni kitabu ambacho kila mwana familia anatakiwa kusoma, kila kijana anayetaka kujikwamua kiuchumi, kila mtu anayejiandaa kustaafu, kila mtu anayetafuta njia ya kulipa madeni na mikopo yake, kila mtu anayetafuta mtaji wa biashara ya ndoto zake na kila mama wa nyumbani.
Ona baadhi ya shuhuda za watu waliopata maarifa ya kitabu hiki
Baraka John
“Naachana na kazi za serikali naanza kufuga kuku wa kienyeji maana nimejifunza mengi sana.”
Mutta J. Mutta
“Hakika umezidi kutonesha kidonda cha ndoto yangu maana naona kama nimechelewa sana ila naamini kwamba niungane na ndugu na wadau wengine tukuombee dua na maombi ili uendelee kutupatia zaidi madini yaliyojificha.”
Patrick Nzunda
“Mafunzo haya ni mazuri sana. Yanajenga wigo mpana wa mawazo ya kimaisha. Ningependa kujua mambo mengi. Asanteni. Mada ya ufugaji wa kuku wa kienyeji imenibariki sana.”
Ritha Msuya
“Nimevutiwa sana kwa kweli inafundisha vizuri na nimetiwa moyo sana na ninamwomba Mungu anisaidie naamini na mimi nitajiajiri kwani nimehitimu chuo mwezi wa nne sasa natumaini nimepata elimu na nitaweza kujiajiri mwenyewe.”
Sebastian Ndohelo
“Hakika somo ni zuri mno kwa mwenye nia ya dhati na aliye tayari kuzingatia maelekezo, nimetiwa moyo. Endelea kutoa elimu muhimu.”
Athumani Mohamedi
“Asante sana nimeupokea ujumbe huu kwa nia ya dhati na nimeanza kujenga mabanda kwa ajili ya mradi wa kuku wa kienyeji.”
Joseph Nelson Kambanga
“Ninapanga kuanza ufugaji wa kuku na tayari nimenunua heka 2 Wilaya ya Kisarawe kwahiyo ujumbe huu umekuwa wa msaada.”
Kitabu hiki hakiongezi orodha ya machapisho kwenye kabati lako bali kinakupa hazina ya ujuzi kichwani na pesa nyingi mfukoni kwako.
Unakosaje nakala yako? Hakikisha vitabu hiki vinafika mkononi kwako.