[Kitabu kipya] Kwanini 'Kwa Heri Chuo Kwa Heri Mafanikio'
Mwandishi wa Kitabu cha Deni la Dhahamu na vingine, Gastor Mtweve amekuja na kitabu kipya. Kitabu cha tofauti chenye mtazamo fikirishi kwa wadau wote wa elimu ya juu na ajira kwa ujumla. Kitabu cha KWA HERI CHUO, KWA HERI MAFANIKIO ni kitabu ambacho hupaswi kukikosa. Kama mzazi mwenye watoto wanaosoma, kijana unayetarajia kwenda chuo, kijana ambaye umehitim chuo, kitabu hiki ni muhimu kwako.
Hiki ni kitabu ambacho kitakupa tafakuri kuhusu mfumo elimu yetu na jinsi ndoto za wahitimu zinavyofifia baada ya kurudi katika uhalisia wa soko la ajira.
Elimu ya chuo kikuu sio elimu ya kila mtu. Katika mafanikio ya kimaisha, wapo watu wanahitaji kuipata elimu ya chuo kikuu na wengine hawahitaji kuipata. Kitabu hiki kitampa msaada mtu ambaye anatarajia kujiunga na chuo kikuu kwa kujitathmini kama anatakiwa kupata elimu hiyo ama la. Ndani ya kitabu kuna maelezo ya kina ya kukuonyesha msomaji “kwa nini sio kila mtu anapaswa kwenda chuo kikuu?”.
Vile vile ndani ya kitabu cha KWA HERI CHUO, KWA HERI MAFANIKIO, mwandishi ameonyesha nini cha kufanywa na mtu ambaye ana elimu ya chuo ambaye hakupaswa kwenda chuo.
Kwa upande mwingine, elimu ya chuo inawajengea wahitimu mtazamo wa maishha mazuri pindi wamalizapo masomo yao, kitu ambacho hakina uhalisia. Kitabu kimeonyesha namna ya kuishi maisha halisi na kubadili mtazamo kwa haraka. Kwa kukosa mwongozo halisi kutoka katika mitaala ya elimu, wahitimu wengi wanaanza maisha halisi ambayo ni tofauti na yale waliyofundishwa na kuaminishwa.
Elimu ya chuo sio kwa ajili ya kila mtu. Watu wengine mafanikio yao makubwa yapo nje ya mfumo rasmi wa elimu. Kwa kutambua kwa usahihi kusudi la kuwepo duniani, utapata jibu sahihi kuhusu mafanikio yako na mchakato wa kupitia ili kufanikiwa.
Kitabu hiki kitakupa njia sahihi za kupita na kutathmini kama mafanikio yako yanategemea elimu ya chuo kikuu ama yapo katika maarifa na ujuzi mwingine. Kila sura ya kitabu hiki imekuja na mtazamo mpya. Mtazamo ambao utamfanya msomaji kufikiria tofauti kuhusu elimu na maisha kwa ujumla.
Credit: Ubunifu wa jalada la kitabu umefanywa na DL Bookstore, angalia huduma zaidi.
Karibu kwa maoni hapa chini.