Soma kozi za bure
Soma kozi za bure kabisa kuhusu uandishi, uchapishaji, na uuzaji wa vitabu. Ni wakati wa kuanza!
Kwa nini usome kozi?
Kozi za uandishi, uuzaji, na uchapishaji zinakufikia moja kwa moja kupitia barua pepe yako. Kozi hizi fupi zimeundwa kukusaidia kuboresha ujuzi wako wa uandishi na uuzaji.
Kozi zinafundishwa na walimu waliobobea na wenye uzoefu mkubwa katika fani zao. Anza siku yako kwa kujifunza jambo jipya linaloweza kukuimarisha zaidi.
Kozi zilizosomwa sana
IFAHAMU MITINDO YA UANDISHI
Kila uandishi una mtindo wake, iwe kuandika riwaya, mashairi, pendekezo na n.k. Katika kozi hii utajifunza; mitindo minne ya uandishi na mambo ya kuzingatia unapoandika kuandika kitabu.
Taught by Daudi Lubeleje
ANDIKA RIWAYA KAMA PRO
Inawezekana umetamani sana kuandika riwaya, lakini hujui pa kuanzia. Katika kozi hii ya siku tano utajifunza mambo mbalimbali ikiwemo: wazo zuri la hadithi hutoka wapi?, nini umuhimu wa ubunifu, mbinu za kuisukuma hadithi na uhariri.
Taught by Esther Karin Mngodo
JIFUNZE UANDISHI WA MAKALA GAZETINI
Kuandika makala gazetini inakupa wigo au uwanja mpana wa wewe kama mwandishi kujitanua katika kazi zako za kiuandishi, na utalifikia kundi kubwa la watu kiurahisi zaidi.
Taught by Linus Siwiti
ANDIKA MASHAIRI KAMA PRO
Katika kozi hii utajifunza, kutaja machache, maana ya ushairi, umbo la shairi, tenzi, msuko, mathnawi, uhuru wa mshairi na kadhalika. Ni kozi ya siku 5 ambayo itakupa ujuzi wa kukuwezesha kuandika mashairi mara umalizapo tu kusoma.
Taught by Omari Juma Kimweri
SANAA YA UBUNIFU WA JALADA NA SAIKOLOJIA YA HADHIRA
KUHARIRI NA KUKIPITIA KITABU
Kitabu chenye makosa kinamwondolea ladha nzuri na tamu msomaji. Kwa hiyo kukipitia na kukihariri kitabu chako ni jambo lisilokwepeka. Inawezekana kitabu kikawa hakina makosa kwa asilimia 100%.
Taught by Daudi Lubeleje
Unapenda kusoma vitabu?
Boresha ujuzi wako wa uandishi, uchapishaji, au uuzaji kwa kusoma kitabu badala ya kusoma kozi. Ni njia rahisi na inayokupa uhuru wa kujifunza kwa kasi yako mwenyewe!
HATUA NNE KATIKA UANDISHI WA VITABU
Unapoingia katika uandishi wa vitabu, au tuseme, unataka kuwa mwandishi wa vitabu, na ni ndoto yako ambayo unataka kuitimiza, kuna hatua ambazo utatembea katika hizo, tunaita hatua katika uandishi wa vitabu..
Taught by Daudi Lubeleje
SIRI NNE ZA KUUZA KITABU NA UKAPATA MAFURIKO YA MAUZO
Kuuza kitabu ni sanaa inayohitaji ufahamu wa kina na mkakati madhubuti. Katika kozi hii ningependa kukushirikisha siri muhimu ambazo zitakusaidia kufikia malengo yako katika uuzaji wa vitabu.
Taught by Daudi Lubeleje