Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support

[Sababu 4] Ugumu wa kuandika kitabu uko wapi?

July 24, 2021 at 2:42 pm,


Watu wengi wanatamani sana kuandika kitabu lakini wanakwama wapi? Kila mtu ukimwuliza kuhusu ndoto yake ya kuandika kitabu atakwambia yuatamani sana kufanya hivyo lakini kwanini tuna watu wachache wanao thubutu kuandika?


Zipo sababu nne ambazo ndiyo kikwazo cha watu wengi kuona uandishi wa vitabu ni kazi nzito na wanashindwa kutimiza ndoto yao ya kuandika kitabu. Sababu hizo ni hizi;

1. Kuanza kuandika bila kuwa na muundo kamili wa kitabu chako vile kitakuwa kikikamilika. Matokeo ya kukosa muundo wa kitabu unachotaka kuandika yatafanya ukose kitu cha kuandika ukiwa katikati ya safari. Kwahiyo ufanye nini sasa? Kabla ya kuanza safari ya kuandika, hakikisha una muunda wa kitabu unayoonyesha ukitoka hapa unaenda hapa halafu unamalizia hapa. Ukifanya hivyo, kuandika linakuwa ni jambo la kufurahia sana.


Soma Makala zingine,

1. Mambo 3 ya kuzingatia kupata jina la kitabulinalouza sana.

2. Njia Nne Za Kumsaidia Muandishi Kuongeza OrodhaYa Imeli [Baruapepe) Za Wasomaji Wake.

3. Hatua tano za kuwatambua wasomaji wako walengwa.

4.  Kwanini mwandishi afanye book cover makeover?


2. Kuanza kuandika kitabu bila kuwa na kusudi kamili la kwanini unaandika kitabu hicho. Kwanini unaandika kitabu hicho? Kama huna majibu, huwezi kujua ni lini utakuwa umemaliza kuandika, tena hutajua kitabu kiwe na nini na nini ndani yake. Kwahiyo anza na kujiuliza kwanini unataka uandike hicho kitabu ili ukikamilisha kusudi hilo na safari ya kuandika inakuwa imekamilika.

3. Una hamasika kiasi gani na kitabu unachoandika?. Kama wewe huna hamasa na unachoandika, Je! Msomaji atakuwa na hamasa?. Kuna msemo unasema “kama kitabu chako hakikutoi machozi, na msomaji wako hakitamtoa machozi”. Sasa ukihamasika kidogo hutaweza hutaweza kumaliza kuandika kitabu chako. Utakosa nguvu ya kuandika kwa weledi na utaona safari ngumu mno. Kwahiyo, kitabu chako kikupe hamasa kubwa wewe na uone kitamsaidia sana kila atakaye kisoma.

Get a Free Ebook

Enter your email to download a free ebook: Hatua 6 za Kuandika Kitabu 

Thank you!

You have successfully joined our subscriber list.

.

4. Kukata tamaa kwa sababu kitabu cha kwanza kilitoka kibaya baya. Kuna yule ambaye ilijikongoja akaweza kuandika kitabu cha kwanza lakini hawezi kuendelea tena kwa sababu kile cha kwanza hakikuwa vizuri. Kwahiyo anaona kuandika ni kugumu sana kwa sababu tu kitabu cha kwanza kilikuwa hovyo. Nikutoe wasiwasi, ni kawaida kitabu cha kwanza kuwa hovyo na haimaanishi kitabu cha pili kitakuwa hovyo pia. Hatua ya kwanza ni ya kujifunza, hatua ya pili ni ya kurekebisha uliyokosea na hatua ya tatu ni ya kukua. Usikate tamaa.

Wewe umekwama kwenye sababu ipi katika hizi sababu nne? andika maoni yako kwenye sehemu ya comments hapo chini. 

Unataka kujua zaidi kuhusu uandishi wa vitabu? Soma kozi bure HAPA na kuwa wa kwanza kupata taarifa za kozi mpya kila inapowekwa.

100% Free courses

Enter your email below and be the first to get our updates about new courses

Thank you!

You have successfully joined our subscriber list.

.



Recent Posts

  • Mambo 10 ya Kujifunza Kutoka Kitabu cha Hamasika Kila Siku
    29 Jun, 2025
  • Download Vitabu 7 vya Fedha (PDF)
    19 Jun, 2025
  • Kutoka Daftari Hadi Kitabu Halisi: Jinsi ya Kugeuza Maandishi Yako Kuwa Kitabu
    16 May, 2025
  • Umechoka na Minyama Uzembe? Suluhisho la Kupungua Uzito Limepatikana!
    17 Apr, 2025
  • Vitabu Bora vya Pasaka vya Kukuimarisha Kiroho – Vinapatikana Sasa DL Bookstore
    11 Apr, 2025
  • 4 Benefits of Selling Your Book Through DL Bookstore
    20 Mar, 2025
  • Download Entrepreneurship Books (PDF) in Swahili
    10 Feb, 2025

selling_book-1.png

Enroll in 100% free courses

100% free courses on writing, publishing, and marketing of books. Time to dive in!

Start learning →

Cart

Cart is empty.

Log in




Forgot password?
Create account
Login to existing account
My orders
My reviews
My details
Log out
  • Home
  • Get books
  • About us
  • Author services
  • Blog
  • Support
  • Client portal
DL Bookstore © 2018 - 2025. All rights reserved.