Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support

Fanya mambo haya 3 uuze sana kitabu chako

August 13, 2021 at 9:38 am,


Ndoto ya kila mwandishi anapoandika kitabu ni kuuza nakala za kutosha. Kitabu chako kinapoingia sokoni unafanya kila unaloweza kiuze na kama hakiuzi lazima ujiulize kwanini. Sasa tujiulize, mafanikio ya mwandishi kwenye kuuza kitabu chake huchangiwa na nini?


Kuna mambo 3 ambayo ukiyafanya lazima kitabu chako kitaua nakala za kutosha, mambo hayo ni haya;

1. Toa kitabu bora. Kuna msemo husemwa kwamba ni msomaji ambaye husema hiki kitabu ni bora. Lakini, wewe kama mwandishi lazima uhakikishe kitabu chako kinatoka bora kuanzia ndani mpaka nje. Hakikisha mchapishaji wako anakitoa kitabu vizuri sana. Huwa inanoga pale msomaji anaposhika kitabu chako, anasema huyu mwandishi alikuwa makini na kazi yake na aliwekeza vya kutosha kupata kazi bora. Inapotokea kitabu chako kimetoka vibaya, msomaji hupata picha ya haraka umelipua lipua hata kama umeandika maudhui bora sana. Jambo la kwanza unapotaka kitabu chako kiuze, fanya kila unaloweza kitabu kitoke vizuri.


Unataka kujua zaidi kuhusu uandishi wa vitabu? Soma kozi bure HAPA na kuwa wa kwanza kupata taarifa za kozi mpya kila inapowekwa.

100% Free courses

Enter your email below and be the first to get our updates about new courses

Thank you!

You have successfully joined our subscriber list.

.

2. Lielewe soko lako vema unalolenga. Ukweli mchungu ambao waandishi wengi huwa hawaukubali ni kuwa kitabu chako hakitapendwa. Kuelewa soko lako ni kuelewa ni wasomaji wa aina gani ulowaandikia. Kitabu chako kinafaa kwa kundi lipi?. Ili ujue soko lako la kitabu litakuwa kwa wasomaji gani unaweza kutumia njia hizi kukusaidia kujua kwa haraka

a. Anza na kuwaangalia waandishi wanaoandika aina ya kitabu kama chako. Mfano, kama unaandika riwaya, angalia waandishi wengine wanaoandika riwaya kama wewe. Kama wasomaji fulani wanapenda vitabu vya DaudiPages basi bila shaka watapenda na vyangu kwa sababu zipo kundi moja.

b. Angalia wasomaji wako wanapatikana wapi zaidi. Si wasomaji wote wako Facebook ama kwa makundi ya WhatsApp, unaweza kuta wasomaji wako ni wale wanaopenda kwenda kununua vitabu kwa maduka ya vitabu. Ukishajua wasomaji wako wanapatikana wapi zaidi, basi hakikisha unawawekea kitabu chako huko ili wakipate kwa urahisi.

Get a Free Ebook

Enter your email to download a free ebook: Hatua 6 za Kuandika Kitabu 

Thank you!

Happy reading!

.

3. Jalada la kitabu liendane na aina ya kitabu ulichoandika. Fikiria umeandika riwaya lakini jalada la kitabu linaonekana kama kitabu cha biashara vile, haitakupa matokeo mazuri sokoni. Ukitaka kuuza nakla nyingi za kutosha, jalada la kitabu chako ni silaha bora ya kuwanasa wasomaji wako.

Karibu kwa comments hapa chini. 



Recent Posts

  • Mambo 10 ya Kujifunza Kutoka Kitabu cha Hamasika Kila Siku
    29 Jun, 2025
  • Download Vitabu 7 vya Fedha (PDF)
    19 Jun, 2025
  • Kutoka Daftari Hadi Kitabu Halisi: Jinsi ya Kugeuza Maandishi Yako Kuwa Kitabu
    16 May, 2025
  • Umechoka na Minyama Uzembe? Suluhisho la Kupungua Uzito Limepatikana!
    17 Apr, 2025
  • Vitabu Bora vya Pasaka vya Kukuimarisha Kiroho – Vinapatikana Sasa DL Bookstore
    11 Apr, 2025
  • 4 Benefits of Selling Your Book Through DL Bookstore
    20 Mar, 2025
  • Download Entrepreneurship Books (PDF) in Swahili
    10 Feb, 2025

selling_book-1.png

Enroll in 100% free courses

100% free courses on writing, publishing, and marketing of books. Time to dive in!

Start learning →

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Get books
  • About us
  • Author services
  • Blog
  • Support
  • Client portal
DL Bookstore © 2018 - 2025. All rights reserved.