Kama mwandishi wa vitabu unataka kufanikiwa kwenye nini?
Chapisho hili tumelitoa katika blogi ya Daudipages
Kuna utafiti nilishiriki hivi majuzi wa Belinda K Griffin kutoka SmartAuthorsLab.com ambao ulitaka kujua, wewe kama mwandishi unataka kufanikiwa kwenye nini? Ulikuwa ni kuchagua moja kati ya majibu haya;
- Kupiga pesa
- Kufikia wasomaji wengi zaidi na ujue vitabu vyako vinapendwa
- Kupata michongo ya biashara
- Kujulikana tu kama nawe ni mwandishi au mtaalamu kwenye eneo unaloandika
- Kushinda tuzo za uandishi
Jibu nililotoa katika utafiti huu ni siri yangu, vipi wewe ungechagua lipi hapo?. Kilichonifanya niandike chapisho hili ni kwamba, Belinda ameshea nami matokeo ya awali ya utafiti huu na yamekuwa ni matokeo ya kushangaza kidogo. Hebu tuone,
- Kuwafikia wasomaji wengi na kujua kwamba wana furahia na kuvipenda vitabu vyako ndiyo jambo kubwa ambalo waandishi wengi wanataka. Utafiti unasema 83.8% ya waandishi walisema wanapenda tu vitabu vyao vifike kwa wasomaji kuliko kupiga pesa na kunufaika na waandishi wao ambayo ilipata 2.7% tu. Je! Kwa sababu waandishi wengi hawataki kupiga pesa kwenye uandishi wao (2.7% tu ya waandishi walisema ndo wanataka), itakuwa ndiyo sababu waandishi wengi hawana pesa ijapokuwa vitabu vyao ni vizuri na watu wanapenda?, au Je! Inawezekana waandishi wanaweka juhudi kidogo sana kwenye kuuza vitabu vyao na wanabaki kufurahia tu kuona kitabu kinapendwa?.
- 86.5% ya waandishi hawarudishi gharama zao za kuandaa vitabu vyao. Pengine hii inaweza sababisha na dhana kwamba, wao wanapenda tu kuona vitabu vinapendwa na wasomaji lakini si kupiga pesa. Lakini jambo la kusikitisha zaidi, 68.4% ya waandishi walisema wao wanajua jinsi ya kufikia malengo yao ijapokuwa nachelea kusema isijekuwa ni ndoto za abunuasi.
Niseme tu kwamba, mimi binafsi nimekuwa nikiwasaidia watu wengi kuwa waandishi waliofanikiwa kwa kuwapa ushauri wa bure, kuandika makala kama hii na mwaka jana mwishoni nilianza kuandaa kozi za kuwasaidia waandishi zaidi. Sasa ikiwa ungetaka usaidizi wangu ili ufanikiwe kwenye uandishi wako na usiwe miongoni mwa 83.8% ya waandishi ambao wana vitabu vizuri lakini hawana pesa, chukua hatua sasa kwa;
- Weka miadi ya kuongea na mimi hapa bure
- Anza kusoma kozi sasa hivi hapa
- Ji subscribe kupata Makala kama hii kwenye baruapepe yako hapa
Karibu kuweka comment yako hapa chini.