- Buy books
- Swahili books
- Fasihi
- Mzimu wa kichaa
Mzimu wa kichaa
“Mzimu wa Kichaa” ni kitabu cha hadithi ya kubuni inayozungumzia nguvu ya mzimu unaosaidia watu wanaoyaishi matendo mema dhidi ya nguvu za giza kwa wana jamii wa kijiji kilichozungukwa na maji ya ziwa. Ubunifu wa hadithi hii unatokana na mkusanyiko wa matukio kadha wa kadha yahusuyo nguvu za giza pamoja na mawazo ya watu wa jinsia, lika na kabira mbalimbali hapa nchini Tanzania.
Usomaji wa hadithi hii utakufanya kuelimika, kuburudika, kusikitika na wakati mwingine kujifunza mambo mbalimbali yanayo sababisha ugumu wa maisha ndani ya jamii inayo kuzunguka na utatuzi wake kwani siyo kila kitu kinachotokea hapa duniani ni mapenzi ya Mungu. Asilimia kubwa, Mungu kamuumba mwanadamu na kumpatia vitendea kazi vyake ambavyo ni akili, macho, mikono, miguu, masikio, mdomo, n.k vitakavyo msaidia kuendelea kimaisha.