Mwanamke na ndoto
Nichukue fursa hii kupitia kurasa hizi kuzungumza na wewe Mwanamke, ikiwa ni njia ya kukufikia ili kukutia moyo, kukuinua, kukupa mbinu zaidi na mpya za kukusadia katika kuzitimiza ndoto zako.
Ninaamini kuwa kila mmoja mmoja kwa imani yake anaamini kuwa anapendwa na Mungu, na kama anapendwa na Mungu basi huyu Mungu anapenda tufanikiwe, Mungu hapendi akuona vile vile kuanzia januari mpaka disemba, hauna mabadiliko, au hali inazidi kuwa mbaya.
Licha ya changamoto mbalimbali za maisha bado ninaamini Mungu anayonafasi kubwa ya kukuwezesha kufanikiwa katika ndoto zako.
Na leo natamani kupitia kurasa hizi, uwe kwenye nafasi ya kuona unafanikiwa, nafasi ya kuona mabadiliko chanya kwenye maisha yako, nafasi ya kuona unafikia malengo yako ungali hai, na hilo ndilo kusudi la Mungu kwako.
Sijui uko katika wakati gani, sijui uko katika sehemu gani, huenda ndio unaanza kujipambania, huenda ndio unamaliza au umerudishwa nyuma au vyovyote vile, kitabu hiki kikawe chachu kwako ya kuona zaidi ya hapo unapoona, ya kufanya zaidi ya hapo unapofanya na ya kufikia ndoto kubwa zaidi ya hizo ulizofikia.
Hii inawezekana lakini kama tukiungana, kama tukiona umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu kwetu kama wanawake, kama tukiona iko sababu ya kuinuana na sio kushushana.
Nikutakie kheri unapoanza kujumuika nami kupitia kurasa hizi, na nimatumaini yangu kuwa utajifunza kitu ambacho kitakujenga na kukufikisha mahali pengine.
Asante kwa kutenga muda wako kujifunza nami, na nikuhakikishie tu kuwa muda wako sio bure, utafaidika kwa uwepo wako hapa.
Kumbuka tu, kundi letu la "Mwanamke Na Ndoto Tanzania - MNT" lipo kwaajili yako na unawezakujiunga na kuunga wengine kupitia namba +255623086786 au nenda Instagram akaunti ya @shwarifoundationafrika, hapo juu utaona "link" itakayokuwezesha kujiunga na group letu na tukaendelea kukua pamoja.
Nisikuchoshe na mengi ila nikukaribishe rasmi katika kujifunza jambo, na nitatarajia kusikia kutoka kwako au hata kukuona siku moja ukiwa umefanikiwa kupitia mafunzo haya.
Asante na Karibu.