Ufanye Nini Uzinduzi Wa Kitabu Chako Unapofeli?
Umeingia gharama kubwa kuandaa uzinduzi wa kitabu chako ukiwa na mategemeo ya kuuza nakala nyingi kama ilivyo kwenye mpango wako uloandaa lakini unapata matokeo yasiyoridhisha, Je! Ufanye nini?. Kufeli kwa uzinduzi wa kitabu chako siyo mwisho wa safari, tumekuandalia mambo matatu ya kufanya ambayo yatarejesha matumaini ya kuuza na kufikia nakala ulizokusudia kufikia
1. Kumbuka jambo hili, watu wengi bado hawajakisikia kitabu chako. Ni kweli hamasa hupungua mara ya kufanya uzinduzi na wengine huanza safari ya kuandika kitabu kingine. Lakini unajua kuwa kuna wasomaji wengi ambao bado hawajasikia kuhusu kitabu chako? Basi jua kuwa wasomaji bado wana haamu ya kupata kitabu chako. Kilicho za zamani kwako, kwa mwingine ni kipya! Kwahiyo kitabu chako bado ni kipya kwa wasomaji hata uzinduzi ukishapita.
Soma pia: Jiunge kwenye kozi zetu za bure za uandishi wa vitabu
2. Usinyamaze! Endelea kuzungumza kuhusu kitabu chako. Endelea kuwakumbusha wasomaji kwamba una kitabu kipya, kipo sokoni. Waambie kwenye mabandiko yako unaandika kwenye mitandao. Jambo la muhimu hapa ni endelea kufanya kila unaloweza kitabu chako kiendelee kuzungumzwa na watu na hayo mazungumzo anzisha wewe.
3. Fanya uzinduzi tena. Ndio! Fanya uzinduzi tena na utashangaa mauzo ya kitabu chako yakipaa juu tena.
Uko tayari kujifunza kozi za bure za uandishi wa vitabu? Jisajili sasa, uwe miongoni mwa watu watakaonza kujifunza kozi za uandishi mwezi huu wa kwanza.