[Podcast] Tips za kukipitia na kukihariri kitabu chako
Kitabu chenye makosa kinamwondolea ladha nzuri na tamu msomaji. Kwa hiyo kukipitia na kukihariri kitabu chako ni jambo lisilokwepeka. Lakini, si waandishi wengi hufanya hivyo. Mara kitabu kinapoingia hatua ya sanifu ya kurasa ndiposa mwandishi anagundua kitabu kina makosa fulani fulani.
Matokeo yake, msanifu anaingia gharama ya kurudia rudia kazi na hata wewe mwandishi unakuwa unapoteza muda ambao ungekuwa kwenye hatua nyingine za kutoa kitabu chako.
Hivyo basi ili kukwepa yote haya, sharti wewe mwandishi au umpatie mhariri ili kukipitia na kukihariri kitabu. Inawezekana kitabu kikawa hakina makosa kwa asilimia 100%. Sasa fuata tips hizi ambazo zitakusaidia wewe kukipitia na kukihariri kitabu chako kwa mafanikio.
- Tips za kukipitia na kukihariri kitabu chako [S01EP01]
- Tips za kukipitia na kukihariri kitabu chako [S01EP02]
- Tips za kukipitia na kukihariri kitabu chako [S01EP03]
- Tips za kukipitia na kukihariri kitabu chako [S01EP04_FINALE]
Kuwa
mwandishi aliyefanikiwa ni maamuzi unayoweza kuyafanya leo kwa kusoma
kitabu hiki UANDISHI WA KITABU KINACHOUZIKA kilichoandikwa na DaudiLubeleje ambaye ameandaa podikasti hizi. Kwa ufupi kuhusu kitabu hiki
Mwenye ndoto ya kuandika na kutoa kitabu ni wewe si mtu mwingine, mwenye ndoto ya kuuza nakala nyingi ni wewe na si mtu mwingine, na mwenye ndoto ya kuwa mwandishi aliyefanikiwa ni wewe na si mtu mwingine. Kwenye hatua yoyote uliyoko sasa; iwe kuandika, kutoa ama kuuza kitabu chako, kitabu hiki kitakuwa msaada kwako.Unapoanza kusoma kitabu hiki unakuwa umeanza safari ya siku 25 za kuwa mwandishi aliyefanikiwa bila stress. Utafanikiwa kutimiza ndoto yako ya kuandika, kutoa na kuuza kitabu chako kwa mafanikio.Upo tayari kuanza siku 25 za kuwa mwandishi aliyefanikiwa?Upo tayari kuandika kitabu kitakachofika kwa msomaji wako?
Ndio! Najua upo tayari,