Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support

Mambo tisa (9) niliyojifunza kwenye uzinduzi wa kitabu cha Jenga Wasifu Wako

July 15, 2022 at 3:33 pm,


Hivi majuzi nilihudhuria uzinduzi wa kitabu cha JENGA WASIFU WAKO kilichoandikwa na rafiki yangu Victor Lazaro (anayeonekana pichani). Uzinduzi huu ulifanyika pale New Safari Hoteli. Yako mengi nilijifunza na ninapenda kukushirikisha machache, kama mambo tisa (9) hivi.


Mambo gani nilijifunza?

  1. Muonekano unaweza kukuangusha lakini uwezo wako hauwezi kukuangusha.
  2. Wasifu unaweza kukupa fursa hata kama huna mtu wa kukutambulisha.
  3. Kipaji na fursa vinaenda pamoja. Unapata fursa kulingana na uwezo.
  4. Watu wanaweza wasikupende kwa muonekano wako. Lakini wanaweza kulipa gharama kubwa kwa sababu ya uwezo wako.
  5. Unamwambia nani uwezo wako? Kuna watu ukiwaambia wataona si kitu, lakini ukisema kwa mwingine inakufungulia fursa.
  6. Muda wa kuongea kuhusu uwezo wako ni muhimu sana. Usiongee wakati hutakiwi kuongea. Soma muda! Soma nyakati!
  7. Uwezo wako uongee. Uwezo wako uongee thamani yako.
  8. Kwa kadiri teknolojia inakua na wewe kua!.
  9. Tunaishi katika ulimwengu unaotaka kuona ni nini unaonyesha. Watu wanataka kuona.

Fun fact: Yesu wakati anachagua wanafunzi alienda nje ya kanisa, hakuchagua waliokuwa kanisani tayari. Fikiria uwezo!

Fun fact: Daudi aliokota mawe matano kwa sababu alijua kuna emergency.

    Ungependa kusoma kitabu hiki cha JENGA WASIFU WAKO? Pakua hapa, Angalia vitabu zaidi hapa

    Nimeandaa kozi ya siku 8 inaitwa SIRI 30 ZA KUWA MWANDISHI BORA ambayo ukiisoma utaweza kufanya mambo yafuatayo;

    ◾ Kuandika kitabu kizuri cha ndoto yako.

    ◾ Kujua namna ya kufikisha kitabu kwa wasomaji wako.

    ◾ Kufanya uzinduzi wa kitabu na kujua namna ya kupanga bei ya kitabu.

    ◾ Kukuza jukwaa lako kama mwandishi.

    ◾ Kupanga bajeti ya kutoa kitabu na kukitoa kitabu chako kwa bajeti finyu utakayokuwa nayo.

    ◾ Utajua jinsi ya kutoa eBook bora kwa wasomaji kwa kuzingatia vitu muhimu

    ◾ Utajua jinsi ya kutengeneza launch team unapotaka kufanya uzinduzi wa kitabu.

    Kozi itaanza mwishoni mwa mwezi huu. Tarehe 30.07.2022

    Jisajili Hapa



    Recent Posts

    • Umechoka na Minyama Uzembe? Suluhisho la Kupungua Uzito Limepatikana!
      17 Apr, 2025
    • Vitabu Bora vya Pasaka vya Kukuimarisha Kiroho – Vinapatikana Sasa DL Bookstore
      11 Apr, 2025
    • 4 Benefits of Selling Your Book Through DL Bookstore
      20 Mar, 2025
    • Download Entrepreneurship Books (PDF) in Swahili
      10 Feb, 2025
    • Download Nine (9) Must-Read Books for Girls and Women 📚✨
      4 Feb, 2025
    • A Tanzanian Platform for Selling Books Online
      4 Feb, 2025
    • Jinsi ya Kuandika Caption Inayochochea Mauzo ya Kitabu Chako
      23 Nov, 2024

    selling_book-1.png

    Enroll in 100% free courses

    100% free courses on writing, publishing, and marketing of books. Time to dive in!

    Start learning →

    Cart

    Cart is empty.

    • Home
    • Get books
    • About us
    • Author services
    • Blog
    • Support
    • Client portal
    DL Bookstore © 2025. All rights reserved.