Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support

#AuthorSpotlight: Tunafurahia mafanikio ya mwandishi Isaack Zake, atoa vitabu vitatu

June 15, 2023 at 12:09 am,


Moja kati ya waandishi wa vitabu ambae tumefanya kazi naye ni wakili Isaack Zake. Mafanikio aliyoyapata kwenye uandishi wake ni hamasa kwa waandishi wengine na sina budi kukushirikisha stori yake ya mafanikio.


Wakati tunaanza kufanya kazi naye, tayari alikuwa keshatoa vitabu kadhaa. Alileta kitabu kimoja kwetu na kazi yetu ilikuwa ni kukifanyia “makeover” kwenye jalada na mpangilio wa ndani. Ile kazi tuliifanya kwa ubora sana na alipokitoa kitabu hiki, mawakili wengi sana walikinyakua haraka. Baada ya uchaguzi wa Raisi wa TLS hapa Arusha, kabla hajaondoka kwenda Dar es Salaam, alinipigia simu akiwa na furaha sana kwa sababu kitabu chake kiliuza mno na kwa ile furaha aliyokuwa nayo aliamua kutupatia kitabu cha pili ili tukifanyie makeover tena. Kufupisha stori, alitupatia na kitabu cha tatu na cha nne (cha nne kilikuwa katika series) ambavyo vyote tulivifanyia makeover.

Vitabu hivi ambavyo tulifanyia makeover kwenye jalada na mpangilio wa ndani vimepata “milestone” mpya. Ni milestone gani hiyo? Isaack ame “donate” vitabu 450 kwa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani. Sasa nikuvute sikio kidogo hapa,

Kama mwandishi, unapata nguvu ya ku “donate” vitabu, ukiacha maudhui bora ya ndani, kama vina jalada la kuvutia na vimepangwa kwa ubora wa juu, na hiki ndicho tulichofanya kwenye vitabu vyake; kumpatia kazi bora, kiasi cha yeye kuamua kutoa vitabu kwa Mahakama yetu. Jambo lingine la ziada ni kwamba, Kwa Isaack ku “donate” vitabu 450 ni moja ya mkakati ambao mwandishi anautumia kufikia “audience” kubwa ya wasomaji wa vitabu, ambao hawa wataweza kununua vitabu vyake vinavyofuata. Haya ni mafaniko makubwa ambayo hatuwezi kuacha kumpongeza Isaack.


Tuje kwako, una kitabu wataka kukitoa? Karibu tukuhudumie. Iwe ni jalada jipya la kitabu au kufanya makeover, wewe karibia na kwa kuanza, tuanzie kuhusu kitabu chako hapa.

_______

Vitabu alivyo donate Isaack ni;

  1. Empoyers’ Common Mistakes under Labour Laws
  2.  How to terminate an employment agreement
  3.   Offences and Penalties under Labour Laws

Hongera Isaack Zake!.



Recent Posts

  • Umechoka na Minyama Uzembe? Suluhisho la Kupungua Uzito Limepatikana!
    17 Apr, 2025
  • Vitabu Bora vya Pasaka vya Kukuimarisha Kiroho – Vinapatikana Sasa DL Bookstore
    11 Apr, 2025
  • 4 Benefits of Selling Your Book Through DL Bookstore
    20 Mar, 2025
  • Download Entrepreneurship Books (PDF) in Swahili
    10 Feb, 2025
  • Download Nine (9) Must-Read Books for Girls and Women 📚✨
    4 Feb, 2025
  • A Tanzanian Platform for Selling Books Online
    4 Feb, 2025
  • Jinsi ya Kuandika Caption Inayochochea Mauzo ya Kitabu Chako
    23 Nov, 2024

selling_book-1.png

Enroll in 100% free courses

100% free courses on writing, publishing, and marketing of books. Time to dive in!

Start learning →

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Get books
  • About us
  • Author services
  • Blog
  • Support
  • Client portal
DL Bookstore © 2025. All rights reserved.