Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support

Mafunzo 10 kutoka kwenye kitabu cha Ushindi Katika Hali Ngumu

December 31, 2023 at 6:11 pm,


Kuna mtu mmoja aliwahi kusema, “Ikiwa tutakutana na mtu mwenye akili adimu, tunapaswa kumuuliza anasoma vitabu gani”. Ukweli wa kauli hii ni kwamba mtu yeyote aliye tofauti anasoma vitabu. Mtu wa kawaida akipita kwenye nyakati ngumu anapigika vilivyo, lakini anayesoma vitabu huwa na mbinu za kuvuka hali ngumu.


Kitabu cha Ushindi Katika Hali Ngumu ni nyenzo yako ya kukusaidia unapopita katika nyakati ngumu, na tumekuandalia mambo 10 ambayo utajifunza ndani ya kitabu hiki. Mambo haya 10 ni kionjo tu kwako, kufahamu zaidi, kitabu hiki kinapatikana hapa.

Haya ndiyo mambo 10 kutoka kwenye kitabu cha Ushindi Katika Hali Ngumu.

  1. “Kama kwa Mungu hakuna jambo gumu la kumshinda na ikiwa tunamwendea yeye ili kutusaidia kutoka kwenye magumu; basi hakuna hali ngumu yoyote ya kuweza kutuzamisha na kutushinda”
  2. “Hali ngumu ni kifungashio cha nje tu cha mambo mazuri”
  3. “Wingi wa ndiyo siyo usahihi wa jambo; usitishwe”
  4. “Tunapitia hali ngumu ili kulipa gharama ya maamuzi ya hovyo tunayofanya kwa kuwasikiliza wengi wanasemaje”
  5. “Bora uchelewe kuliko kuwahi ikiwa unakoenda bado hujajiridhisha vya kutosha”
  6. “Raha ya kushinda changamoto ni kubwa kuliko raha ya kukosa changamoto”
  7. “Utamu wa stori si maneno bali ni ushindi kwenye magumu
  8. “Kaa kuanzia asubuhi mpaka jioni ukilalamika, ikifika jioni nitakuuliza swali rahisi, ‘umebadilisha nini ulivyomaliza kulalamika?”
  9. “Ukweli wa maisha ni kuwa unayemtegemea kukutoa wewe kwenye hali ngumu, yeye pia yuko katika hali ngumu yake”
  10. “Ushindi huanza na kutengenezwa toka ndani ya mtu ma si nje ya mtu”

Soma zaidi ya haya mambo 10, pakua kitabu cha Ushindi KatikaHali Ngumu hapa.

Karibu kwa comments hapa chini



Recent Posts

  • Kutoka Daftari Hadi Kitabu Halisi: Jinsi ya Kugeuza Maandishi Yako Kuwa Kitabu
    16 May, 2025
  • Umechoka na Minyama Uzembe? Suluhisho la Kupungua Uzito Limepatikana!
    17 Apr, 2025
  • Vitabu Bora vya Pasaka vya Kukuimarisha Kiroho – Vinapatikana Sasa DL Bookstore
    11 Apr, 2025
  • 4 Benefits of Selling Your Book Through DL Bookstore
    20 Mar, 2025
  • Download Entrepreneurship Books (PDF) in Swahili
    10 Feb, 2025
  • Download Nine (9) Must-Read Books for Girls and Women 📚✨
    4 Feb, 2025
  • A Tanzanian Platform for Selling Books Online
    4 Feb, 2025

selling_book-1.png

Enroll in 100% free courses

100% free courses on writing, publishing, and marketing of books. Time to dive in!

Start learning →

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Get books
  • About us
  • Author services
  • Blog
  • Support
  • Client portal
DL Bookstore © 2025. All rights reserved.