Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Gharama ya kubarikiwa
Waamini wengi hawajui kwamba sehemu ya agano walilonalo na Mungu ni ahadi ya kubarikiwa na kuishi katika baraka isiyo na kikomo. Pamoja na hilo, wapo watu wengi sana walio na tafsiri isiyo sahihi kuhusu baraka ndio maana kila siku wanapambana kutafuta maisha badala ya kufurahia maisha. Bwana Yesu alipokuja alitangaza kwamba yeye ndiye Bwana wa Sabato (Pumziko).
Kitabu hiki kimebeba siri na ufunguo utakaokusaidia kupata pumziko katikati ya dunia yenye taabu na masumbufu mengi. Baraka ya Bwana huachilia akili, maono na mawazo yasiyo ya kawaida, huzalisha imani thabiti inayoweza kuvuta visivyoonekana vikaonekana. Inatoa nguvu ya kuthubutu mambo makubwa, uwezo wa kuvumilia na kungojea; na kibali kinachokupa upendeleo usiostahili na mpenyo wa kupita pasipopitika. Baraka isiyozuilika inakufanya uwe mtu asiyezuilika.