Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
HILI NI NENO LA KUFAA KWAKO - Siku 21 za kukua, kujijenga na kujiimarisha kiroho
Matokeo ya kusoma kitabu hiki yapo wazi; ukue, ujengeke na ujiimarishe kiroho. Badala ya kuwa mkristo goigoi, legelege na usiyetumainiwa, uwe mkristo mkomavu ambaye utategemewa na Bwana, kanisa lako na watu wanaokuzunguka.
Si afya kabisa kwamba wewe ni mkristo wa muda mrefu lakini umedumaa kiroho, hukui na huleti manufaa kwenye ufalme wa Mungu.
Sasa,
Kitabu hiki kinalenga kukupa hatua ya kuanza kuelekea badiliko lako la kiroho. Kimejaa maandiko ya kutosha na mifano iliyofafanuliwa kwa lugha nyepesi mno. Unapoanza kukisoma leo, hutakiweka chini kwani utatamani uendelee mpaka ukimalize.
HILI NI NENO LA KUFAA KWAKO kwa sababu maisha yako yatabadilika mno na nitakuwa nasubiri ushuhuda wako mpendwa. Hizi ni siku 21 za kukua, kujijenga na kujiimarisha kiroho.
Upo tayari kuanza siku ya kwanza sasa hivi? Usichelewe, sasa anza!