Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Ifahamu Biblia Vizuri
Ni raha sana kusoma kitabu ambacho unajua kimeandikwa na nani, lini, kwa nini, kwa ajili ya nani na wahusika wake ni akina nani.
Kwa mfano, kitabu cha Ruthu kimeandikwa na Nabii Samweli. Matukio ya Ruthu yalitokea wakati fulani kati ya 1160 KK na 1100 KK, wakati wa kipindi cha mwisho cha waamuzi (Ruthu 1:1). Lakini kitabu cha Samweli mwenyewe hakikuandikwa na Samweli kwa sababu sura ya 25 ya Samweli wa kwanza inaelezea kifo cha Samweli. Unaweza kuona kwamba ingekuwa ngumu mtu kuandika habari za kifo chake wakati kinatokea. Sasa ni nani aliandika? Ndio maana uko na kitabu hiki mkononi mwako.
Kitu kimoja nina uhakika nacho ni kwamba ukisoma kitabu hiki utaona raha kusoma Biblia na utaipenda zaidi. Ufahamu wako kuhusu Mungu na Biblia utaongezeka sana kwa sababu nusu ya maswali yako yotr uliyonayo kuhusu Biblia majibu yake yako ndani ya kitabu hiki