Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Ishara 12 za kuwatambua manabii na waalimu wa uongo
Suala linalohusu kuwatambua manabii na waalimu wa uongo, limekuwa linaleta shida sana kwa watu wengi, kwa sababu manabii na waalimu hao wa uongo wanapokuja kwa watu kuleta ujumbe wao hudai “tumetumwa na Mwenyezi Mungu kuleta ujumbe wake na hivyo kuwataka wanadamu kuupokea, kuuamini na kuufuata”.
Inapotokea nabii au mwalimu amekuja kwa mtindo huo na akakutana na watu wasiojua kuwapambanua manabii na waalimu kwa misingi ya Neno la Mungu, ndipo ukengeufu hutokea, na makundi ya aina mbalimbali ya imani za uongo hujitokeza. Hivyo lengo la kitabu hiki ni kukupa maarifa katika msingi wa Neno la Mungu, kuweza kuwatambua manabii na waalimu wa uongo.