Kanuni ya Kuishi Maisha ya Utele
Maisha ya utele huja kwa mtu binafsi kujishikamanisha na Mungu wa utele kwa tabia ya utoaji inayobebwa na maisha ya utakatifu na uadilifu kwa Mungu. Mith 28:20. “Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; ……..” Mith 10:22. “Baraka ya Bwana hutajirisha…….” Mw 22:16-17. “akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, 22 : 17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;”
Kupitia kitabu hiki utaweza kujifunza “UTOAJI” utajua sababu, kanuni, faida na hasara. Yafuatayo ni baadhi ya mafundisho utayojipatia ndani ya kitabu hiki.
- Chanzo cha baraka na maisha ya utele .
- Chanzo cha wazo la baraka ni nani? .
- Sehemu ya Mungu katika mapato yako.
- Sababu kuu 13 za mwanadamu kumtolea Mungu sadaka mbalimbali.
- Hasara “saba” zinazompata mtu bahili – asiye mtolea Mungu.
- Sadaka isiyopokelewa na Mungu wala kulipwa .
Aina 8 za sadaka zilizo muhimu kwa mkristo.
- Sadaka ya malimbuko.
- Sadaka ya zaka / fungu la kumi.
- Sadaka ya changizo.
- Sadaka ya kumtokea Mungu.
- Sadaka ya nadhiri
- Sadaka ya shukurani.
- Sadaka kwa mtu “watu” (kuwahudumia wahitaji / ukarimu).
- Sadaka ya kuitoa nafsi yako mwenyewe .