Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Maisha ya ushindi kwa kijana mkristo
“Maisha ya ushindi kwa kijana mkristo” ni ujumbe uliobeba mawazo na makusudi mema kabisa ya Mungu juu ya maisha ya kijana mwamini wa Yesu Kristo. Mwandishi anatushirikisha mambo kadhaa muhimu ambayo kijana yeyote mkristo anapaswa ayafahamu na kuyazingatia ili aweze kuona kusudi la Mungu juu ya maisha yake linatimia na hivyo kuwa mshindi katika maeneo mbalimbali yahusuyo maisha yake.
Katika kitabu hiki, mwandishi kwa msaada wa Roho mtakatifu ameelezea siri iliyojificha juu ya nguvu na uthamani wa kijana katika ulimwengu wa roho, na namna ambavyo vijana wengi wakristo wameshindwa kuishi maisha ya ushindi kwasababu ya kutokufahamu nguvu iliyomo ndani yao na umuhimu/uthamani wao katika familia ya wakristo.
Kitabu hiki ni msaada kwa vijana wakristo katika kuweza kujitambua vyema na kuweza kuishi maisha ya ushindi.