Mbinguni na Jehanum
Kitabu hiki ni kitabu ambacho kimebeba siri kubwa kuhusu Mbinguni na Jehanum. Katika maisha yetu ya sasa, wanadamu tumekuwa ni kama tumejisahau kwa sababu ya umbali wa safari tuliyotoka. Wapo wengine ambao wanafikiri wameshafika tayari walikokuwa wanaelekea, lakini kumbe bado tuko safarini.
Katika kitabu hiki, ninamshukuru Mungu ambaye amenipa utulivu wa kupitia Biblia na kugundua uwepo wa vituo vikuu viwili ambavyo safari yetu itaishia huko na magari yetu yanaenda huko yaani Mbinguni na Jehanum. Kwa kweli kitabu hiki ni kitabu ambacho ninatamani kila mmoja akisome kwa nia ya dhati kabisa kwani kinaenda kuwavuta watu wengi kwa Mungu na kulisababisha lile gari linaloenda Jehanum liwe tupu kabisa.
Ninakushauri kitabu hiki soma wewe pekee yako, na familia yako, na kila mtu unayempenda kwani ni mapenzi ya Mungu kuwa sote tuende kwake tukakae naye milele. Hivyo ni vizuri kama utamshirikisha na mwenzako kitabu hiki na kitakuwa cha baraka sana kwenu nyote. Jipatie kitabu chako sasa.
Others Also Bought