Mungu anakupenda
Sababu iliyomsukuma Mungu kumtoa mwanaye wa pekee ulimwenguni ilikuwa ni kule kuupenda ulimwengu. Mungu aliupenda ulimwengu kiasi kukubwa chenye thamani ya mwanaye wa pekee.
Mungu aliupenda ulimwengu; hakuchagua rangi, kabila, au jinsia, aliupenda ulimwengu wote. Watu wa kila kabila, na lugha, na jamii. Kila rangi na kila mtazamo wa kimawazo.
Kutokana na upendo, Mungu anaudhihirisha wema wake kwa wanadamu wote. Na ni wema wa Mungu pekee wenye uwezo wa kumfanya mtu kugeuka, kumwelekea, kumfuata na kumpata Mungu (Warumi 2:4).
Recommended for you

Nuru ya Upendo
TZS 5,000