Namna ya Kushughulika na Roho Chafu, Laana na Minyonyoro ya Uovu
Umefundishwa kwamba ukiwa ndani ya Kristo hauko chini ya LAANA tena, ni kweli HAUKO CHINI ya laana. Sio kila laana bali ni laana ya torati. Biblia iko very clear (Galatians 3:13 ), hauko chini ya laana ya dhambi kwa sababu Yesu alilipa matakwa yake kwa kifo chake Msalabani. Sasa kuna kitu kinaitwa LAANA ya UKOO, hii Yesu hakuiondoa kwa sababu matakwa yake ni wewe kuwa sehemu ya huo ukoo. Yesu alichofanya, ni kukupa UWEZO wa kuikabili (Marko 16:16).
Hii haiondoki automatically kwa sababu uko ndani ya Yesu kwa sababu kuwa ndani ya Yesu hakuondoi ukweli kwamba wewe ni sehemu ya huo ukoo. Ukitaka kunielewa kirahisi hebu geuza laana ya ukoo kuwa UTAJIRI wa ukoo. Kama kwenu kuna utajiri wa ukoo, kuwa kwako ndani ya Yesu hakukuondoi kuwa mnufaika wa huo utajiri wa ukoo. Na wakijaribu kukutoa kwa sababu eti uko ndani ya Yesu utawashitaki na hiyo kesi utashinda. Kwa sababu kigezo cha kupata huo utajiri ni kuwa ndani ya huo ukoo sio kuokoka. Mapepo ya kwenu yanajua kwamba umeokoka lakini huo mzigo wa LAANA umeandikwa jina la ukoo wenu.
Maadam wewe ni wa huo ukoo yatakuletea na kukufikishia kwa uaminifu. Kitakachoamua kwamba hizo laana zinakuchakaza au la sio kuwa kwako ndani ya Yesu bali ni kiasi gani wewe ni IMARA KATIKA BWANA NA KATIKA UWEZA WA NGUVU ZAKE. (Efeso 6:10).
UHODARI wako katika Mungu (Neno) na NGUVU (Maombi) zake hakuondoi laana za UKOO kwako, bali kunakufanya wewe uwe na NGUVU JUU YAKE. Kwa hiyo zikija kwako zinakutana na nguvu kubwa, na ulimwengu wa ROHO unaitika kwenye nguvu sio mamlaka. Ndio maana Yesu ametupa vyote nguvu na mamlaka. Ndio maana mchawi mwenye bidii anaweza kumloga mzee wa kanisa mvivu kuomba na akafa. Ingawa mzee ana mamlaka kuliko mchawi. Mamlaka sio nguvu bali ni UHALALI wa kutumia nguvu.
Ukiwa na mamlaka lakini hauna NGUVU, Ukikutana na watu wasio jali mamlaka, watakumaliza. Mkuu wa majeshi asiyejua kupigana akikutana na vibaka wasio na utii kwa mamlaka yake, wanaweza kumuua. Ndio maana kuna watu wameokoka na bado magonjwa yanawatesa. Kuendela kusema kwamba siko chini ya laana wakati haujui Sanaa ya vita za kiroho, ni sawa na kujifunika uso wakati simba yuko mbele yako ili asikuue. UTALIWA. Yesu alishughulika na magonjwa pia, kwa kupigwa kwake tu liponywa.
Umewahi kujiuliza kwanini watu wako ndani ya Yesu na bado wanateswa na magonjwa. NI SANAA YA VITA RAFIKI YANGU. Inakuwaje Yesu alifanyika masikini ili sisi tuwe matajiri lakini bado watu wako ndani ya Yesu na wamebarikiwa na baraka zote za rohoni lakini bado ada za shule zinawatoa jasho. NI VITA MURAH. Haya mambo yamekamilika ndio lakini sio huku duniani, ni katika ulimwengu wa ROHO. Na teknolojia ya kuyafanya yale Yesu amefanya katika ulimwengu wa ROHO yawe halisi katika ulimwengu wa mwili, inaitwa Efeso 6:10-13
Yesu alimshinda Shetani kihalali lakini shetani ni mwana wa kuasi, hajali hayo mambo na ameachiwa huku duniani. Ni mpaka shetani umzuie kwa nguvu ndio anaondoka sio tu kwa kuwa ndani ya Yesu. (Yakobo 4:7)
Nakutia moyo pata maarifa ya SANAA ya vita za Rohoni.
Others Also Bought


