Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Yaishi Maisha Katika Wokovu
Kitabu hiki ambacho ni toleo la kwanza la huduma ya BJL, kimebeba ujumbe maalum kwa ajili yako mpendwa ambaye umekwisha pokea wokovu na sasa unasafiri duniani kwenda mbinguni kwa Baba.
Unayeona fahari kuupokea wokovu kama maandiko yanavyosema, "Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako, Uliouweka tayari machoni pa watu wote" Lk 2:30-31 SUV na ambaye sasa umeamua kuishi maisha mapya ndani ya Kristo kama maandiko yanavyosema, "Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye;" Kol 2:6 SUV
Ndani ya kitabu hiki utapokea mafundisho ya Neno la Mungu juu ya wokovu namna ya kuyaishi maisha ya wokovu, ikiwa pamoja na kuifahamu toba ya kweli, umuhimu wa ubatizo, kuishi sawasawa na Neno la Mungu na kudumu katika maombi.
Niseme tu wazi kwamba mambo mengi katika wokovu ni magumu sanalakini ukisoma kitabu hiki utagundua waziwazi kwamba siyo wewe tena anayeishi na kuyafanya hayo mambo magumu bali Kristo aliyeko ndani yako. Utagundua kuwa utu huu mpya tuliyoupokea katika Kristo ni wenye nguvu za Mungu ndani yake.