Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Chura wa Kijeshi
Hapo mwanzo chura alikuwa na muonekano mzuri sana, ngozi nyororo na sauti yenye mvuto wa kipekee, hakika alivutia.
Chura huyu alijaliwa kuwa na vipaji vingi mojawapo ya vipaji hivyo lni utambaji wa hadithi loo alikuwa na hadithi tamu sana. Hadithi zake zilijaa mafunzo na maonyo ya kutosha. Chura alikuwa na umahiri wa hali ya juu katika kufikisha ujumbe kwa wasikilizaji wake kwani aliongea kwa madaha na kutoa msisimko wa kipekee kwa wasikilizaji kiasi cha kufanya watu wengi wampende na kutembelea makazi yake.
Lakini nyuma ya sifa zote nzuri za Chura huyu kulikuwa na siri nzito! Chura alikuwa mwanaharakati, nyuma ya harakati hizo kulikuwa na agenda. Fuatana na mtunzi kupata uhondo zaidi.