Hamasika Kila Siku
Kufanya kitu kimoja kwa kukirudia, ndio kitu kigumu ambacho kina changamoto kubwa katika kuleta mabadiliko ya watu wakati wa kuchukua hatua kwenye maisha ya kila siku. Kwani tafiti zinasema, watu wengi wanaweka malengo mwanzo wa mwaka, kufikia tarehe 19 ya mwezi wa kwanza, nusu ya watu wanakuwa tayari wamesahau na kuachana na malengo ambayo walikuwa wameyaweka mwanzo wa mwaka.
Ukifuatilia kwa kiasi kikubwa, kitu kinachosababisha mwendelezo huo kukwama ni hamasa inayokosekana katika kufanya kitu cha mwendelezo wa kila siku hata kwa hatua kidogo kabisa.
Msingi wa kitabu hiki cha Hamasika kila siku ni kukuchambulia kila eneo la maisha ambalo linatuzunguka na kukutengea tafakari 366; ambazo ni moja kwa siku; namba za mwaka mrefu ambao unatokea kwenye mzunguko wa mwaka. Ukiweza kusoma na kuandika kila siku angalau tafakari moja na kuisoma mfululizo, kitu hicho kimoja tu kinakwenda kuleta mabadiliko kwenye maisha yako. Kwani tabia moja ndogo inaleta athari kwenye vitu vingine unavyovifanya kwenye maisha yako.
Licha ya kila mtu kutamani mafanikio kwenye maisha, lakini ni wachache sana walioshinda katika hili. Sababu kubwa inayotofautisha makundi haya mawili, si nyingine bali ni uthubutu wa kuchukua hatua na mwendelezo.
Nikupongeze kwa hatua kubwa na muhimu uliyoichukua ya kukipata kitabu hiki endelea kukisoma ili kujipatia mahitaji Hamasa muhimu ya kila siku kukuwezesha kupata mafanikio makubwa. Naamini hutajutia maamuzi yako ya kukipata kitabu hiki, nakutakia kila la kheri katika usomaji na uchukuaji hatua.