Ishi ndoto yako
Je, umewahi kuhisi kuwa kuna ndoto kubwa ndani yako—ndoto ambayo inaita, lakini hofu inakuzuia kuijibu? Je, umewahi kuota maisha ya maana, yenye kusudi, lakini kila mara unapojaribu kupiga hatua, sauti ya mashaka, aibu au hofu ya kushindwa inakurudisha nyuma?
Kitabu hiki ni mwongozo wa kiroho na kimaisha kwa kila mtu anayetamani kuishi kwa lengo aliloumbiwa. Ishi Ndoto Yako hakielekezi tu jinsi ya kufikia ndoto zako, bali kinagusa kiini cha safari ya kweli—kuondoa minyororo ya hofu, kupona ndani yako, na kuamka kwa ujasiri mpya wa kuishi kwa kusudi la Mungu.
Kwa kupitia sura 10 zenye mashiko, kitabu hiki kinakusaidia:
- Kutambua ndoto iliyo ndani yako
- Kufunua chanzo cha hofu na jinsi ya kuishinda
- Kuijua sauti ya Mungu kuhusu maisha yako
- Kuelewa hatua za vitendo za kutimiza ndoto yako
- Kujifunza kutokana na mifano ya watu walioishi ndoto zao licha ya vikwazo
Hiki si kitabu tu, ni mwaliko wa kuamka na kuanza kuishi maisha yako kikamilifu—maisha yaliyojaa ujasiri, kusudi, na tumaini. Ikiwa umewahi kujiuliza, “Je, ndoto yangu itatimia kweli?” basi hiki ndicho kitabu chako.
SABABU YA KUANDIKA
“Niliandika kitabu hiki kwa moyo mzito baada ya kuona watu wengi wanaishi maisha ya mazoea, huku ndoto zao zikiangamia kwa sababu ya hofu. Ndoto yako si ndoto tu—ni sauti ya kusudi lako la kipekee. Usikubali iishie kuwa wazo. Ishi ndoto yako.”
Recommended for you

