Jirani Yangu
Kitabu hiki ni zao la swali ambalo Yesu aliulizwa kuhusu Jirani. Hii habari katika Vitabu vya Injili unaweza kuichukulia kwa wepesi lakini kupitia kitabu hiki tutaieleza habari hii kwa kina kuhusu Jirani.
Hiki ni kitabu ambacho kinaenda kujibu maswali mbalimbali ambayo watu tumekuwa tukijiuliza kuhusu Jirani, na kwa kila atakayejitoa kikamilifu kujifunza yaliyomo katika kitabu hiki, hakika hatabaki kama alivyokuwa kwani Roho Mtakatifu amenipa ufunuo huu kwa ajili ya kulisaidia kanisa lake.
Majirani tunao katika kila mahali tunapoenda, na tunapaswa kujua jinsi ya kuishi nao, na wakati mwingine sisi pia ni majirani wa watu wengine, hivyo tunapaswa kuwa na maarifa mapana juu ya namna tunavyoweza kuishi pamoja nao kwa ajili ya utukufu wa Mungu katika jamii zetu.
Ndani ya kitabu hiki yapo mengi unayoenda kujifunza, hivyo nina kila sababu ya kuombea ufahamu wako ili Mungu akusaidie uweze kuelewa mafundisho haya na yawe na faida katika maisha yako. NIMEKUOMBEA KWA MUNGU, ILI AKUPE NEEMA YA KUELEWA HAYA NA KUYAFANYIA KAZI.
Others Also Bought