Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Kwako binti ambaye bado hujaolewa
Kumekuwa na wimbi kubwa la changamoto katika mahusiano, ndoa na hata malezi.
Changamoto hizi zimewakumba wengi na miongoni mwa kundi ambalo limeathirika ni mabinti. Kuna walioolewa ambao wanatamani watoke kwenye ndoa, na kuna ambao hawajaolewa wanatamani kuingia kwenye ndoa.
Wapo walioolewa ambao wanatamani muda urudi nyuma warudie kipindi cha kabla ya kuolewa na wapo ambao bado hawajaolewa ambao wanaona kipindi cha kabla ya kuolewa ni kama laana au hakifai kuwepo kabisa. Kuna ambao wameolewa na bado wanajiona wapweke, na kuna ambao hawajaolewa wanataka kuolewa ili waondoe upweke. Kuna sababu nyingi ambazo zimepelekea mambo kuwa hivyo ikiwemo mitazamo katika jamii.
Ndani ya kitabu hiki, mwandishi
amefafanua na kuelezea sababu zinazowafanya mabinti wengi kuathirika na mambo
hayo, na pia ameeleza ni nini binti anapaswa kufanya ili kuukomboa wakati na
kuutumia vizuri kabla hajaolewa na hata baada ya kuolewa ili aishi maisha yenye
faida na sio hasara katika kipindi cha yeye kuishi hapa duniani.