Maajabu ya Bidii
Katika maisha watu hutamani mafanikio ya kila namna lakini si wote wanafikia malengo hayo. Na inawezekana kabisa wana jitahidi kwa bidii ili kufikia malengo yao lakini wanakwama kwa sababu ya ukosefu wa bidii ya kweli inayoongozwa na maono sahihi, maarifa, na uvumilivu.
Kitabu cha Maajabu ya Bidii kimeandikwa ili kumsaidia msomaji kuelewa kuwa bidii peke yake haitoshi kama haijaambatana na mambo kadhaa wa kadhaa kama vile nidhamu binafsi, na msingi wa kiroho.
Mungu wetu ametupa zawadi ya bidii lakini kama ilivyo mbegu, inahitaji kupandwa kwenye udongo mzuri ili izae matunda. Watu wengi wanafanya kazi kwa bidii lakini hawaoni matokeo kwa sababu hawana maono yanayoongoza juhudi zao, hawana maarifa ya kuyasimamia mafanikio yao, au hukata tamaa kabla ya kufikia kile walichokusudia.
Aidha, kitabu hiki kinaelezea kwa undani jukumu la bidii katika kukuza uzao wa kiungu, kikionesha wajibu wa wazazi na walezi katika malezi yanayozalisha kizazi kinachomcha Mungu na kuishi kwa kusudi.
MAAJABU YA BIDII Wakati huo huo, kitabu kimeelezea namna ya Kushinda Uvivu, jambo ambalo linatoa mwanga na hatua za vitendo za kumsaidia msomaji kujitambua, kubadili mtazamo, na kujenga tabia ya kufanya kazi kwa bidii bila visingizio.
Lengo lililo nyuma ya kitabu hiki ni kukuamsha, kukutia moyo, na kukuongoza ili uone kuwa bidii iliyo sahihi na jinsi inavyoweza kuleta matokeo katika maisha yako. Karibu usome, ujifunze, na ugundue maajabu yaliyofichwa ndani ya bidii
Others Also Bought