Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Mwingine sio wewe
Wewe ni mtu ambaye Mungu amekuumba kwa kusudi lake na kwa ajili yake japo watu wengi tumejisahau na tumekuwa tukidhani tupo duniani kwa kusudi la kufanya na kutimiza ndoto zetu tu na wengine hatujui tutakwenda wapi na tutafanya nini lakini cha ajabu kabisa ni kwamba wapo wasiojua hata wapo kwa ajili ya nini na kwa kusudi gani? Wapo tu na wanaishi na hawajali chochote kile.
Ukweli ni kwamba tumeumbwa kwa kusudi maalumu na lengo maalamu kila mtu yupo kwa kusudi lake ili alitimize yeye kama yeye na kila mtu analo kusudi lake la pekee la yeye kuwapo katika sayari hii ya dunia hata mapacha hawako na kusudi sawa licha ya kwamba wamezaliwa pamoja japo Mungu anaweza kukupa watu wakukufanikishia jambo lako hiyo haina maana wao hawana kusudi ndani yao la hasha wengine kusudi lao laweza kuwa ni kuhakikisha wengine wanafanikiwa kupitia wao, na wengine kusudi lao laweza kuwa ni kuajiri, wengine kuwa wanamichezo wakubwa, wengine kuwa wataalamu wa picha za mnato,wengine kuwa viongozi wa wenzao n.k