Unlock your 15% off discount
Get any book you would love to read for almost free!
Naandikaje kitabu?
Kitabu hiki ni toleo lililoboreshwa la kitabu cha Mbinu Rahisi Za Kuandika Kitabu. Wakati nilipotoa kitabu cha Mbinu Rahisi Za Kuandika Kitabu nililenga kuwasaidia watu wanaotaka kuingia kwenye uandishi wa vitabu lakini hawana watu wa kushika mkono ili kufanikisha ndoto zao. Lengo bado ni lile lile isipokuwa nimeboresha zaidi na kufanya marekebisho fulani fulani baada ya kupokea maoni kutoka kwa wasomaji wengi waliosoma kitabu.
Katika toleo hilo jipya, nimeongeza vitu vingi ambavyo naamini, unapokisoma kitabu hiki utatoka ukiwa na nguvu mpya ya kuandika kitabu chako na hatimaye kutimiza ndoto yako ya kuwa mwandishi wa kitabu. Naandikaje kitabu? Ni swali ambalo nimejibu katika kurasa zinazofuata. Mimi naamini, kuandika kitabu ni ujuzi ambao kila mtu anawez kujifunza
Anza kusoma!