Nguvu Nyuma ya Maandalizi Binafsi
Mtu yeyote ambaye amekusudia au anatamani siku moja watu wamtambue kwenye eneo ambalo ameitwa kulitawala (eneo analotamani kufanikiwa nalo) huwa haishi kama vile ambavyo watu wengine ambao hawana kiu ya mafanikio wanaishi.
Na moja ya kitu ambacho kinamtofautisha mtu anaye yatazamia mafanikio na yule ambaye hajui anapokwenda na ameyakatia tamaa maisha yake ni kwenye eneo linaitwa MAANDALIZI BINAFSI.
Mafanikio ya mtu mwenye maandalizi ni jambo ambalo si la kushtukiza wala la kushangaza kwasababu maandalizi ni utabiri wa kesho tukiwa bado tupo leo. Yaani hauhitaji kiongozi wa dini wala mtumishi wa Mungu aje kukutabilia kwamba utamiliki mali na utakuwa mtu mkuu. Kwasababu hii ni kanuni ambayo Mungu mwenyewe aliiweka tangu kuwekwa kwa misingi ya dunia hii. Ila kama hauna maandalizi binafsi na unasema unataka mafanikio utakuwa unatudanganya na hatuwezi kukubaliana nawewe, na hata kama ikitokea ukafanikiwa basi mafanikio yako yatakuwa na mipaka na mwisho wake yataanguka tu. Huko mbele utakwenda kujua kwanini nasema hivi.
Sifa kubwa ya kanuni yeyote ile ni kumfanikisha mtu yeyote yule anaye ifuata bila kujali ni mtu wa namna gani, (hata kama hamjui Mungu unaye mwamini wewe) bado atafanikiwa na wewe ambaye unamjua Mungu na haufuati KANUNI HII tarajia kufeli. Yaani kiufupi naweza kusema hivi Kanuni haimtupi anayeifuata.
Nakupongeza sana kwakujipatia nakala laini ya kitabu hiki kwasababu hakitakuacha kama ambavyo ulikuwa kabla ya kukisoma kwani kitabadilisha kabisa mtazamo wako kwenye maeneo yote ya maisha na kitakufanya uchukue hatua ya kutenda hata kabla haujakimaliza.
Kwenye hiki kitabu utakwenda kujifunza mambo mengi yahusuyo maandalizi ikiwemo tafsiri yake sahihi, ulazima wa kujiandaa kwa mtu mwenye kesho kubwa, umuhimu wa watu kwenye maandalizi yako, nafasi ya watu waliokutangulia kwenye mafanikio yako, dhana ya kazi na kufanya kazi pamoja na mambo mengine mengi sana.
Haujapoteza muda, bando na pesa yako kuwa na kitabu hiki. Karibu tuanze pamoja.
Others Also Bought


