Nguvu ya umoja katika kundi
Kuna kauli inasema, "Kidole kimoja hakivunji chawa". Kauli hii inaweza kuonekana ya kawaida sana na wakati mwingine inaweza hata kupuuzwa na kuonekana kuwa imepitwa na wakati. Lakini si kweli, kwani Mungu mwenyewe anathamini sana umoja kati ya mtu na mtu (Zaburi 133:1-3).
Kitabu hiki, Mungu alinipa mahususi kwa ajili ya kanisa lake pamoja na vikundi mbalimbali vilivyomo ndani ya kanisa. Katika kitabu hiki utajifunza mambo ya muhimu katika safari yetu ya kurudi kwa baba.
Baadhi ya mambo utakayojifunza katika kitabu hiki ni pamoja na;
- Kwa nini tujifunze kuhusu Umoja katika Kundi?
- Nini kinachoweza kuharibu umoja?
- Nini kifanyike ili kurudisha umoja uliopotea?
- Hasara za kukosa Umoja,
- Faida za kuwa na Umoja.
Kupitia kitabu hiki, utaona jinsi ambavyo Mungu anaguswa sana na Umoja wa watu waliokusudia kufanya jambo kwa ajili ya utukufu wake. Ni kitabu ambacho kimebeba hazina kubwa na kina umuhimu kwa kila mtu anayetamani kuyafikia malengo yake kwa kiwango kinachostahili na alichokusudiwa nacho. Jipatie nakala yako.
Others Also Bought