Vizazi vya baraka
Katika nyakati hizi ambazo misingi ya familia nyingi inatetereka, kuna haja ya kurudi haraka katika kusudi la Mungu juu ya familia na vizazi. Nilipata msukumo wa kuandika kitabu hiki baada ya kuona pengo kubwa kati ya watoto na wazazi, kati ya kizazi cha sasa na kweli halisi ya kimungu.
Kila ninapotazama jamii, ninasikia kilio kisichoelezeka, kilio cha watoto wanaohitaji uelekeo, na kilio cha Mungu akiuliza, "Je, nitawaambia watu wangu juu ya mipango yangu, nao watawaamuru watoto wao kunifuata?". Kitabu hiki kimebeba mzigo wa moyo wangu kuhusu hatima ya vizazi vyetu.
Pia, kitabu hiki kinaakisi imani yangu kwamba mabadiliko ya jamii huanzia kwenye mabadiliko ya familia. Hakuna taifa linalojengwa bila watoto, na hakuna watoto wanaojengwa bila malezi yenye msingi wa kiroho ndani yake. Mungu hana mpango wa muda mfupi, huwa anawaza kizazi baada ya kizazi na hivyo mzazi aliye na mtazamo wa mbinguni lazima afikiri kwa mujibu wa vizazi, si siku chache tu.
Kitabu hiki nimeandika kwa lugha rahisi, lakini yenye uzito wa maandiko na ufunuo wa kiroho. Ni matumaini yangu kuwa kila mzazi, mlezi, kiongozi au mwalimu atapata mwongozo, faraja na changamoto ya kusimama tena katika nafasi yake si kwa hofu, bali kwa imani. Mungu aliye mwanzilishi wa familia, bado yuko tayari kuwasaidia wale wote wanaotamani kulea vizazi vya baraka, si vya huzuni. Na huu ndio mwito wa kitabu hiki. Jipatie nakala yako sasa.
Others Also Bought