Mahusiano 707
Mahusiano 707 ni mkusanyo wa majibu ya maswali yanayoulizwa sana kuhusu upendo, mapenzi, ndoa, na mahusiano. Pastor Bedon Dickson anachambua changamoto za kawaida zinazowakumba watu katika maisha ya kimapenzi na kutoa mwanga wa kiroho, kimaadili, na kiushauri ili kusaidia wasomaji kufanya maamuzi sahihi.
Kwa kutumia misingi ya Biblia na uzoefu wa maisha halisi, kitabu hiki kinawafaa wale wote wanaotafuta kuelewa maana ya mahusiano ya kweli na jinsi ya kuyajenga kwa uimara, heshima na hekima. Ni msaada muhimu kwa vijana, wachumba, wanandoa, na washauri wa ndoa.