Mambo 26 Yaboreshayo Thamani Ya Mke Kwa Mumewe Ili Kumzuia Asitoke Nje Ya Ndoa.
Ni kitabu kinacholenga kuelimisha mwanandoa jinsi ya kuilinda ndoa yake, kimesheeni ujuzi wa faragha na ujuzi wa kawaida kuhusiana na maisha ya kila siku ya mwanamke aliyeolewa. Migogoro na talaka hutokana na ufahamu duni kuhusu maisha ya ndoa. Kuna mambo mengi katika kitabu hiki baadhi yake ni haya yafuatayo:
Mwanamke anaweza kumteka mumewe asitoke nje ya ndoa kwa:
- Adumu katika nafasi yake (wajibu) kwa kufahamu kuwa “kichwa bila mwili au mwili pasipo kichwa siyo mtu kamili”
- Aitike kama “MSAIDIZI”(mshauri wa mumewe)
- Amwonyeshe mumewe faida ya uwepo wake.
- Amwonyeshe mumewe kwamba, ameumbwa kwa ajili yake.
- Amwonyeshe mumewe ukaribu kwa mgusano wa mwili.
- Amwonyeshe mumewe wema wake kwa matendo maalum.
- Amwonyeshe ujuzi mumewe katika kuyaweza mapenzi.
- Asikose hekima ya kuwakilisha mjadara kwa njia ya upole, upendo na uwazi.
- Atambue kuwa hakuna kitu bora mbadala kwa nafasi yake katika moyo wa mumewe.
- Awaze kudumisha nia njema, na amani.
- Awe kimbilio, mlezi na faraja kwa mumewe.
- Awe mtu wa kuaminika.
- Kinywa chake kijae maneno ya kutia moyo.
- Kuwa msafi (Mwenye mvuto kwa mwonekano wa nje).
- Nguvu ya mwanamke katika mafanikio ya mumewe.
- Utoaji wa zawadi ni tabia ya kusisimua.
- Uwazi wa kushirikisha mipango yake kabla ya utendaji.
Others Also Bought
Barua ya Siri kwa Wanandoa Wote