Tabia 28 Zinazo Boresha Thamani Ya Mke Kwenye Mahusiano Ya Ndoa
Mke mwema hujitanabaisha kwa kutunza heshima ya mume wake, hujipambanua kwa kudumu katika maisha yake halisi, hutambua “AINA YA KAULI” inayofaa masikioni mwa mumewe,huchochea “Dalili” zinazomtambulisha kuwa mke wa mtu, hutoa kauli na ishara ya kumtaka mumewe kwa ajili ya tendo la ndoa, ni mkarimu na mcheshi kwa mumewe, huwa na adabu na heshima kwa mumewe, hutambua jitihada za mumewe na “Kumpongeza na kumtia moyo”, hujitolea kuwa “Faraja” kwa mumewe, huwa na hekima katika maamuzi yake, hajitambulishi kwa uvivu, ni mshauri mzuri wa mumewe, hawezi kuthubutu kushindana na mume wake, huwa na uwezo wa kuthibiti hisia zake, huwa na utayari wa kukabiliana na mabadiliko, hujitahidi sana kudhibiti hasira kali inayojaribu kumhimiza kususa wajibu wake wa ndoa, hujizuia na tamaa, hapendi kuchochea ugomvi nyumbani wala kumkwaza mume wake, hakosi sauti ya kushukuru katika sikio la mumewe, hujitahidi kuzuia kila viashilia vinavyoweza kuwa chanzo cha ukosefu wa amani kakika familia yake, huomba kibali kwa mume wake kabla ya kuchukua hatua za utendaji, huzingatia na kudumisha usafi wa mwili wake na mazingira ya makazi yake, huwa tayari kukosolewa na mume wake bila kukasirika na kususa shughuli husika.