Una Wito wa Ndoa Kabla ya Ndoa?
NDOA ndio taasisi kongwe zaidi kuliko hata DINI iliyokusudiwa na Mungu idumu milele. Ni agano linalomuunganisha mtu MUME na mtu MKE kiroho na kimwili katika KUTIMIZA KUSUDI LA MUNGU ndani yao.
Najua umeshawahi kujiuliza kwa nini leo hii tunashuhudia MIGOGORO mingi katika taasisi hii takatifu ya ndoa? Kuna sababu nyingi sana zinazoweza kupelekea wanandoa kuachana (TALAKA) ama kuuana, lakini sababu mojawapo kubwa ni ukosefu wa UFAHAMU na MAARIFA kuhusu MAHUSIANO na NDOA kwa ujumla wake.
Ukweli ni kuwa wengi wetu tumejengewa mawazo kuwa maisha ya ndoa ni ya matatizo tu, naamini hata leo hii bado wengi wanafikiri hivyo, wamepokea hivyo, ndio maana kila anayeoa au kuolewa lazima aambiwe kuwa nenda kavumilie. Sijui wewe rafiki yangu uliambiwaje? Sikiliza, si mpango wa Mungu ndoa iwe sehemu ya mateso au iwe ni sehemu ya matatizo yanayopelekea watu kukosa amani na hata kupata magonjwa na kufa; au kushindwa kumtumikia Mungu wao.
Niliamua kuandika kitabu hiki kwa ajili ya wale wote wanaojitayarisha kufunga ndoa, wale walio kwenye ndoa tayari, na kwa yeyote anayetamani kupata ufahamu zaidi kuhusu maisha ya ndoa. Kwa sababu tunaishi katika siku ambazo talaka zimekuwa nyingi na utata mwingi kuhusu suala hili.
Ni tumaini langu kupitia kitabu hiki nitaweza kukusaidia kuchochea imani yako na uhakika wa maisha mazuri yenye upendo kwa wale ambao bado hawajaanza safari ya ndoa na wale walio tayari katika ndoa. Nakutia moyo tena kuwa inawezekana tena kutengeneza upya hadithi yako nzuri katika maisha ya ndoa kwani NDOA NI MPANGO ASILI WA MUNGU!
NAMALIZIA kwa kukumbusha kuwa pamoja na yote ambayo umekuwa unayasikia na kuyafahamu kuhusu ndoa, lakini niamini NAPOKWAMBIA kuwa ndoa ni nzuri hasa kama MWANAUME (mtu mume) na MWANAMKE (mtu mke) watajifunza na kuzifuata KANUNI ZA ASILI (Laws of nature) kabisa zilizowekwa na Mungu mwenyewe kuhusu taasisi hii kongwe kuliko zote DUNIANI.
Others Also Bought


