Jarida la bure | Maisha Jinsi Tuyajuavyo
Mshairi wa uingereza W.H .Auden anasema "tumewekwa duniani kusaidia wengine lakini kile wengine wamewekwa kukifanya siwezi kusema". Watu wengi hufikia hatua ya kukata tamaa na kushindwa kabisa kustahimili nilimsikia mtu mmoja akisema "Nimedhoofika sana,nimeumwa sana maisha yangu yamekuwa ya mateso mno hapa duniani ,nikapumzike tu. Huzuni na dhiki haitakuwepo tena,sitaomba omba mahitaji"
Watu wengi hufikia hatua ya kukata tamaa na
kushindwa kabisa kustahimili nilimsikia
mtu mmoja akisema "Nimedhoofika sana,nimeumwa sana maisha yangu yamekuwa
ya mateso mno hapa duniani ,nikapumzike tu. Huzuni na dhiki haitakuwepo
tena,sitaomba omba mahitaji"
Kamwe tusimpite mtu anayeteseka bila
kujitahidi kumpa faraja,kama sisi tulivyopewa tulipokuwa katika hali hiyo. Kuna
mengi yakutunyong'onyeza, na kutufanya tuhisi upweke mkubwa mno. Magonjwa
yanatufanya kuwa dhaifu sana, unaweza kuwa mzima leo, kesho ukawa kitandani hoi
,unapigania maisha.
Kuna wakati tunapitia magumu mengi ya kutisha kiasi cha kushindwa kujua
tufanyaje zaidi ya kuwa na hofu .Hatujui kesho yetu imebeba nini ? tutakuwa
wapi ? tutakuwa na hali gani? nani
atakushika mkono na kurejesha lile tumaini angavu? . Mwinjilisti Pascal Cassian
anasema " Hakuna mtu anayejua kesho yake,hata mimi sikujua kama ningekuwa
hivi ,kama ningelijua nitakuwa hivi ningejiandaa,ningeweka akiba nisije
ombaomba"
Mwandishi Joyce Mayer anasema "Hebu
fikiria jinsi ambavyo ulimwengu, ungelikuwa na tofauti iwapo kila mmoja wetu
angefanya jambo la ukarimu kwa mtu fulani kila siku . Matokeo yake yangekuwa ya
kushangaza.Ulimwengu ungebadilika haraka..Fanya sehemu yako watu wengine
watafanya sehemu yao.Usikubali ushindwe kupitia kufikiri kabla hujaanza."
Ukiwa kweli unataka kitu fulani chenye manufaa
kwa watu wengine ,utatafuta njia ya kufanya.Hakuna zawadi ya kutofanya lolote
,fanya kitu.Huwezi kuwa masikini kwa sababu tu ya kuwasaidia wengine.Usiseme
huna uwezo wa kuwa shughulikia watu wengine sababu labda kipato chako ni kidogo
. Mama Teresa anasema"hakuna mtu ambaye ni masikini mpaka hana kitu cha
kutoa...". Kama uwezi kufanya mambo makubwa wewe mwenyewe ,kumbuka unaweza
kufanya mambo madogo kwa maana kubwa.Kuna mambo mengine mengi ,muhimu na ya
thamani unayoweza kufanya yenye mguso mkumbwa kwenye maisha na kuleta tofauti
ifaayo ulimwenguni kupitia mambo madogo madogo ."Tumia resilimali zako
,zaidi ya pesa .Resilimali zetu ni pamoja na nguvu , wakati ,vipawa,na mali
tulizonazo"anasema Mwandishi wa mageuzi ya upendo Joyce Mayer........
BURE BURE BURE BURE…JIPATIE JARIDA LETU LA
MAISHA JINSI TUYAJUAVYO TOLEO LA PILI JIHUSISHE FANYIKA BARAKA. BURE
ILIKULIPATA
WASILIANA NASI 0624006306 au email
maishajinsituyajuavyo@gmail.
Ubunifu wa jalada na mpangilio wa ndani wa jarida hili umefanywa nasi DL Bookstore. Angalia huduma zetu HAPA
Kununua vitabu vya kusoma tembelea HAPA