NJIA MBILI MUHIMU ZA KUUZA KITABU KWA MASHABIKI WAKO
Unapoandaa mpango wako wa kuzindua kitabu, kuuza kitabu chako kwa mashabiki wako liwe ni jambo la kwanza. Kuna njia nyingi unaweza tumia kumnasa shabiki wako anunue kitabu chako. Kati ya njia hizo, kuna hizi chache za kuanzia;
1. Mpe zawadi kwa shabiki wako. Usiseme kwa shabiki wako nunua kitabu changu kipya halafu ukaishia hapo, endelea kumwambia, ukinunua kabla ya tarehe fulani utapata bure kitabu changu fulani kama zawadi yako au ukinunua kitabu changu utapata mwezi mmoja bure wa kujiunga na kozi yangu fulani. Jambo la muhimu hapa ni shabiki apate kitabu na zawadi yako ambayo itakuwa nyongeza yake.
2. Fanya kampeni kwa kutumia imeli. Ili kutumia njia hii lazima uwe na orodha ya imeli za mashabiki wako. Kitangaze kitabu chako kwa kutumia imeli utakazotuma kwa mashabiki wako. Isiwaandikie nunua kitabu changu, la! Wape sehemu ya kitabu chako bure, mfano sura ya kwanza na watanunue ili kusoma sehemu iliyobakia. Usitume imeli nyingi, angalau kwa wiki, tuma imeli kuanzia tatu mpaka nne.
Lengo la “uza kwa mashabiki” wako kama sehemu ya kwanza katika uzinduzi wa kitabu ni; (i) inakusaidia kila mtu kujua kuhusu kitabu chako kwamba kimetoka na kinapatikana (ii) inakusaidia kumfanya mashabiki aseme hapana kununua kitabu chako.