Unatamani kuandika kitabu? Fuata hatua hizi 4
Unatamani kuandika kitabu lakini unakwama? Tumekuandalia hatua hizi nne rahisi za kukusaidia wewe kutimiza ndoto yako ya kuandika kitabu chako. Fuata hatua hizi nne,
1. Anza na kujiuliza kwanini unataka kuandika. Je! Unataka kuongeza uandishi kama chanzo cha kujipatia kipato?, Je! Unataka kutimiza ndoto ya maisha ya kuwa mwandishi?, Je! Unataka kutoa majibu ya changamoto fulani kupitia kitabu utakachoandika?
Tip: Andika chini angalau sababu tano kwanini unataka kuandika kitabu.
2. Chagua tanzu unayotaka kuandikia. Tanzu za uandishi ziko nyingi, mfano, riwaya ambazo tena zimegawanyika zaidi, kuna riwaya za taharuki, mapenzi, na n.k, kuna biashara, siasa, taaluma. Wewe unataka uandike kwenye tanzu ipi?
Tip: Angalia kipaji chako kinakuelekeza wapi. Angalia ni wapi pale unapoandika unafurahia na kuona wepesi zaidi.
PAY LESS, MORE BOOKS
Get any book you would love to read for almost free!
3. Fanya mazoezi ya kuandika sasa. Uandishi unataka uandike. Andika na chapisha kwenye mitandao ya kijamii, makundi sogozi ya WhatsApp na n.k
Tip: Usihofie kuhusu utakachoandika. Anza kuandika utajikosoa baadaye
4. Kusanya ulichoandika na ongeza maudhui zaidi. Chagua katika vingi utaandika, hasa vile utapewa mrejesho na wasomaji wako, kusanya, fanya uhariri na ukipata kurasa 30+ boooom! Kitabu tayari
Tip: Uandishi huwa unakua, utaanza na hatua sifuri baadaye utafika hatua 100, usiogope kitabu kitapokelewaje, wewe toa kitabu.
Ukweli mchungu ni kuwa si kila mtu atapenda kitabu chako. Lakini jambo la uhakika, utakuwa na watu watakaopenda vitabu vyako. Hao wakupe hamasa ya kuandika zaidi na utaendelea kuwa bora kwenye uandishi.
___
Kujifunza zaidi, unaweza kusoma kozi hii;
Au kozi hii;
Karibu kwa maoni yako kwenye comments