Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Books
  • Publish
  • Sell
  • Courses
  • Blog
  • Support

Unaisomaje kozi ya Siri 30 Za Kuwa Mwandishi Bora Wa Vitabu?

July 25, 2022 at 4:05 pm,


[Kutoka DaudiPages] Zikiwa zimesalia siku chache mno – Siku 5 tu, kozi itaanza tarehe 30.07.2022 – kozi ya Siri 30 Za Kuwa Mwandishi Bora Wa Vitabu kuanza, nimeona nigusie jambo hili; Unaisomaje kozi hii?. Nifanya hivi nikitambua kuwa kuna watu wengi, ikiwemo wewe, wanajiuliza hivi nitaisomaje kozi hii?. Natambua fika kabisa ratiba yako inaweza kuwa inabana, huna muda au una dharura na inakupa ukakasi kuamua uisome kozi au uiache.


Baada ya kusoma mpaka mwisho hiki ninachokwenda kuandika naamini utabadilisha mawazo na kuamua kujisajili na kuisoma kozi hii.

Nianze sasa,

1. Utahitaji nini kusoma kozi hii?. Ili kusoma kozi hii utahitaji mambo matatu tu!; simu yako, baruapepe yako, na bando lako.

2. Unaanzaje kuisoma kozi?. Ni rahisi sana, nitakupatia link na nywila (pasiwedi) yake ya kuingia kwenye kozi. Ili kukuondolea adha ya kuingia mara kwa mara kwenye kozi (ku log in), kozi hii imeandaliwa kwa namna ambayo utaingia mara moja tu siku ya kwanza ambapo hapo hapo (instantly) utapokea mada ya kwanza na kisha katika siku zitakazofuata hutahitaji tena ku log in isipokuwa mada zitakuwa zinakuja zenyewe kwenye baruapepe yako automatically, si nzuri sana hii jamani!.

3. Uwasilishaji wa kozi. Kozi hii utaisoma kupitia simu yako na mada za kozi zitakufikia kupitia baruapepe yako. Hii itakupa urahishi wa kuisoma hata ukiwa kwenye gari, daladala, ukiwa unatembea au hata unapika jikoni kwako!. Unafungua tu baruapepe yako na kuanza kusoma.

4. Muda wa kuisoma. Hii ni moja ya kozi inayoitwa “self-paced course” kumaanisha kwamba, unaisoma wakati wowote kwa wewe mwenyewe kuamua muda wa kuanza kuisoma. Mfano, unaweza kuamua kuisoma muda wa asubuhi, hivyo kila siku asubuhi utapokea mada ya kozi, au utasema mimi napendelea kusoma mchana, basi kila siku mchana utapokea mada ya kozi, hali kadhalika ukichagua usiku iwe ndiyo muda wako wa kusoma kozi, utapokea mada muda huo.

Jambo la muhimu zaidi kufahamu ni kwamba, muda ule ule utakaopokea mada ya kwanza katika siku ya kwanza, ndiyo utakuwa muda wa kupokea mada zote katika siku zitakazofuata; kwa mfano, unaamua kuanza kusoma kozi leo saa sita mchana, basi kesho saa sita mchana utapokea mada ya pili, vivyo hivyo na kesho, kesho kutwa mpaka mwisho wa kozi.

Haya pengine unajiuliza, vipi kama nitapokea mada halafu nikakosa muda wa kuisoma? Relax! Kwa sababu unapokea mada kwenye baruapepe yako, mada zote zitabaki kwenye baruapepe yako na wakati wowote tu unafungua na kuanza kusoma.

5. Utolewaji wa mada za kozi. Mada zitafundishwa katika mfumo wa maandishi na sauti (audio). Hii itakupa uhuru wa kuamua kusoma au kusikiliza, raha iliyoje!. Kila siku unapata mada moja tu! Kwenye baruapepe yako, na hii itakusaidia kujifunza vizuri na kufanyia kazi yale utajifunza.

6. Kujibu mazoezi. Kozi hii ina maswali mwishoni mwa mada. Ki-msingi, swali linaloulizwa ni swali la takafari ili kuku – engage wewe kwenda hatua mbele zaidi katika kile ulichojifunza. Sasa, majibu ya maswali utayatuma kwa ku – reply email au kwenye kijisehemu cha kutuma majibu ambacho kitakuwa mwishoni mwa mada

5. Cheti cha kozi. Kozi hii ina cheti cha kumaliza kozi ambacho utapata mwishoni mwa kozi baada ya kujibu mtihani mfupi wa ku – reflect yale umejifunza. Hiki utatumiwa katika baruapepe yako.

Baada ya kozi nini kinafuata? Baada ya kozi nitaendelea kukusaidia kwa kadiri utakavyohitaji usaidizi wangu. Naamini utakuwa na maswali ya kuniuliza, kutaka ushauri na kadhalika, hivyo tutaendelea kuzungumza. Mwisho wa kozi, si mwisho wa mimi na wewe kuongea.

Nini cha ziada? Usichelewe kujisajili kwenye kozi kama bado hujafanya hivyo, BONYEZA HAPA kujisajili kwenye kozi. Kama tayari umekwisha kujisajili, basi relax! Subiri kuanza tu!, ikifika tarehe 30 utapokea link na pasiwedi ya kuingia kwenye kozi kwenye namba yako ya simu.

Bado una maswali? Andika kwenye comment hapa chini



Recent Posts

  • Tumia mbinu hizi rahisi na uwe miongoni mwa 1% wanaomaliza kusoma vitabu
    5 Dec, 2025
  • Faida za Kuhariri Kitabu kwa Waandishi na Njia za Kukamilisha Uhariri
    1 Dec, 2025
  • Ukitumia njia hizi, utapenda kusoma vitabu
    27 Nov, 2025
  • Siri 5 Unazopaswa Kujua Kutoka Kitabu: Jilipe Mwenyewe Kwanza
    10 Jul, 2025
  • Mambo 10 ya Kujifunza Kutoka Kitabu cha Hamasika Kila Siku
    29 Jun, 2025
  • Download Vitabu 7 vya Fedha (PDF)
    19 Jun, 2025
  • Kutoka Daftari Hadi Kitabu Halisi: Jinsi ya Kugeuza Maandishi Yako Kuwa Kitabu
    16 May, 2025

selling_book-1.png

Enroll in 100% free courses

100% free courses on writing, publishing, and marketing of books. Time to dive in!

Start learning →

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Books
  • About us
  • Publish
  • Sell
  • Blog
  • Support
DL Bookstore © 2025. All rights reserved.