Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support

Umuhimu wa kuandaa bajeti ya kutoa kitabu

September 19, 2022 at 3:36 pm,


Unaujua umuhimu wa kuandaa bajeti kwanza unapokuwa kwenye mchakato wa kutoa kitabu chako? Fikiria una rafiki yako ambaye amekuja kwako kuomba ushauri wa kuifanya bajeti yake ya kutoa kitabu itoshe, Je ungemshauri nini?.


Hili ni swali ambalo niliwauliza wanafunzi waliosoma kozi ya Siku 30 Za Kuwa Mwandishi Bora. Katika wanafunzi waliosoma kozi hii, yupo Emmanuel Chifunda ambaye nilipenda sana majibu yake kiasi cha kuona niya-publish hapa ili na wewe uweze kujifunza.

Emmanuel Chifunda alijibu swali hili kama ifuatavyo;

Nimejifunza umuhimu wa kuandaa au kuwa na bajeti kwanza katika mchakato wa kutoa kitabu. Ushauri nitakao mpa rafiki yangu ili kuiweka sawa hiyo bajeti kusudi aendelee na mchakato wa kutoa kitabu chake ni kama ifuatavyo:

  1. Alipie gharama kwa kufuata mtiririko wa vipaumbele. Hapo nitamshauri aanze na usanifu bora wa jalada la kitabu chake.

  2. Afanye mwenyewe zile shughuli ambazo atakuwa na ujuzi nazo ili kupunguza gharama.

  3. Alinganishe bajeti yake na gharama za wachapishaji mbalimbali wa vitabu.

  4. Ili kupunguza gharama ya kupata ISBN, afuatilie moja kwa moja kutoka Maktaba ya Taifa kuliko kununua kwa mchapishaji.

Baada ya majibu haya, nilihamasika sana kujua kama Emmanuel Chifunda ameshatoa kitabu chake na aliniambia ametoa kitabu cha kwanza kizuri sana. Kitabu alichoandika kinaitwa Ishara 12 za kuwatambua manabii na waalimu wa uongo ambacho kwa ufupi wake, ameandika kwamba;

Suala linalohusu kuwatambua manabii na waalimu wa uongo, limekuwa linaleta shida sana kwa watu wengi, kwa sababu manabii na waalimu hao wa uongo wanapokuja kwa watu kuleta ujumbe wao hudai “tumetumwa na Mwenyezi Mungu kuleta ujumbe wake na hivyo kuwataka wanadamu kuupokea, kuuamini na kuufuata”. Inapotokea nabii au mwalimu amekuja kwa mtindo huo na akakutana na watu wasiojua kuwapambanua manabii na waalimu kwa misingi ya Neno la Mungu, ndipo ukengeufu hutokea, na makundi ya aina mbalimbali ya imani za uongo hujitokeza. Hivyo lengo la kitabu hiki ni kukupa maarifa katika msingi wa Neno la Mungu, kuweza kuwatambua manabii na waalimu wa uongo.

Kitabu hiki unaweza kukisoma kupitia hapa.

Je! na wewe ungetaka kusoma kozi hii ya Siku 30 Za Kuwa Mwandishi Bora? Bonyeza hapa kuanza kusoma kozi hii.

Credit: DaudiPages

Karibu kwa maoni hapa chini.





Recent Posts

  • Umechoka na Minyama Uzembe? Suluhisho la Kupungua Uzito Limepatikana!
    17 Apr, 2025
  • Vitabu Bora vya Pasaka vya Kukuimarisha Kiroho – Vinapatikana Sasa DL Bookstore
    11 Apr, 2025
  • 4 Benefits of Selling Your Book Through DL Bookstore
    20 Mar, 2025
  • Download Entrepreneurship Books (PDF) in Swahili
    10 Feb, 2025
  • Download Nine (9) Must-Read Books for Girls and Women 📚✨
    4 Feb, 2025
  • A Tanzanian Platform for Selling Books Online
    4 Feb, 2025
  • Jinsi ya Kuandika Caption Inayochochea Mauzo ya Kitabu Chako
    23 Nov, 2024

selling_book-1.png

Enroll in 100% free courses

100% free courses on writing, publishing, and marketing of books. Time to dive in!

Start learning →

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Get books
  • About us
  • Author services
  • Blog
  • Support
  • Client portal
DL Bookstore © 2025. All rights reserved.