Skip to main content
DL Bookstore
  • Home
  • Get books
  • Author services
  • Courses
  • Blog
  • Support

Vitabu vya lazima kusomwa na wanawake na mabinti

November 2, 2023 at 8:28 pm,


Mwanamama Louisa May Alcott ambaye ni mwandishi wa kitabu cha Rose in Bloom anasema “Endelea kuwa na watu wazuri, soma vitabu vizuri, penda vitu vizuri na isitawisha nafsi na mwili kwa uaminifu uwezavyo.”

Ukweli huu anaosema Louisa huonekana kwa Dhahiri pale wanawake na mabinti wanaposoma vitabu. Hivyo basi tumekuandalia orodha hii ya vitabu ambavyo ni lazima kusomwa na wanawake na mabinti.


1. Mwanamke na ndoto. Sijui uko katika wakati gani, sijui uko katika sehemu gani, huenda ndio unaanza kujipambania, huenda ndio unamaliza au umerudishwa nyuma au vyovyote vile, kitabu hiki kikawe chachu kwako ya kuona zaidi ya hapo unapoona, ya kufanya zaidi ya hapo unapofanya na ya kufikia ndoto kubwa zaidi ya hizo ulizofikia.


Hii inawezekana lakini kama tukiungana, kama tukiona umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu kwetu kama wanawake, kama tukiona iko sababu ya kuinuana na sio kushushana.

Soma kitabu


2. Mambo 11 kutoka kwa wanawake waliofanikiwa. Je! wanawake waliofanikiwa zaidi wana mambo gani ya ziada? Kitabu hiki kitakupa maarifa ya kujua kuhusu wanawake waliofanikiwa

Soma kitabu 

3. Barua kwa binti. "Barua Kwa Binti" ni ujumbe ambao natamani sana kuufikisha kwako, "BINTI", ujumbe ambao ukiuelewa, huenda ukakufaa sana katika maisha yako, ujumbe ambao binafsi sikupata pengine bahati ya kuusikia nikiwa kama wewe na pengine nilijifunza mengi mwenyewe kwa kadri nilivyokua nikikua.


Ninatambua yako mambo mengi ambayo umeyasikia, na hasa ukizingatia ni ulimwengu wa teknolojia, au pengine wewe unabahati ya kuwa na waalimu wengi waliokuzunguka, lakini naamini bado iko nafasi ya kujifunza, maana ambapo hukupita yupo anaepitia hapo na kujifunza toka kwake si ujinga

Soma kitabu


4. Kwako Binti ambaye bado hujaolewa. Ndani ya kitabu hiki, mwandishi amefafanua na kuelezea sababu zinazowafanya mabinti wengi kuathirika na mambo hayo, na pia ameeleza ni nini binti anapaswa kufanya ili kuukomboa wakati na kuutumia vizuri kabla hajaolewa na hata baada ya kuolewa ili aishi maisha yenye faida na sio hasara katika kipindi cha yeye kuishi hapa duniani.

Soma kitabu

Angalia vitabu zaidi 



Recent Posts

  • Umechoka na Minyama Uzembe? Suluhisho la Kupungua Uzito Limepatikana!
    17 Apr, 2025
  • Vitabu Bora vya Pasaka vya Kukuimarisha Kiroho – Vinapatikana Sasa DL Bookstore
    11 Apr, 2025
  • 4 Benefits of Selling Your Book Through DL Bookstore
    20 Mar, 2025
  • Download Entrepreneurship Books (PDF) in Swahili
    10 Feb, 2025
  • Download Nine (9) Must-Read Books for Girls and Women 📚✨
    4 Feb, 2025
  • A Tanzanian Platform for Selling Books Online
    4 Feb, 2025
  • Jinsi ya Kuandika Caption Inayochochea Mauzo ya Kitabu Chako
    23 Nov, 2024

selling_book-1.png

Enroll in 100% free courses

100% free courses on writing, publishing, and marketing of books. Time to dive in!

Start learning →

Cart

Cart is empty.

  • Home
  • Get books
  • About us
  • Author services
  • Blog
  • Support
  • Client portal
DL Bookstore © 2025. All rights reserved.