Historia ya Mitume wa Yesu na Vifo vyao
Biblia katika Waefeso 2:20 inasema, "Mmejengwa juu ya msingi wa Mitume na Manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jengo lote linaunganishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu kwa Bwana. Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja na kuwa maskani ya Mungu katika Roho" Kuwafahamu na kuwaelewa Mitume wa Yesu ni jambo ambalo halikwepeki, kwa kuwa kanisa "limejengwa juu ya msingi wa Mitume na Manabii".
Pia, hata Wakristo wa Kanisa la kwanza walidumu katika fundisho la Mitume. Tunasoma katika maandiko hivi, "Wakawa wakidumu katika fundisho la Mitume...." katika Matendo 2:42. Mitume hawa hawa walichaguliwa na Bwana Yesu mwenyewe ili wawe kiungo kati yake na waumini wake ulimwenguni mwote, wakikabidhi mafundisho yake na kushuhudia maisha yake yote tangu ubatizo wake hadi kifo chake na kipekee zaidi kufufuka kwake.
Walitakiwa kukubali kufa kwa ajili ya ushuhuda huo na ndivyo walivyofanya katika kulitimiza agizo hilo. Hata sisi leo, Biblia inatutia moyo na kutuagizavkuwa na ujasiri huo huo kama uliokuwa ndani ya Mitume kwani Bwana Yesu aliahidi kuwa nasi hata ukamilifu wa dahari. Katika kitabu utajua maisha ya kila mwanafunzi wa Yesu, jinsi alivyoitwa, huduma yake na jinsi alivyokufa.
Kumbuka, Biblia inataja vifo vya wanafunzi wawili tu ambao ni Yuda Iskariote na Yakobo Mkubwa, mwana wa Zebedayo lakini wale 10 hakuna mahali Biblia inataja vifo vyao, lakini kupitia kitabu hiki utafahamu hayo yote na mengine mengi. Jipatie kitabu chako uyajue mambo mengi usiyoyajua kuhusu Wanafunzi wa Yesu.
Others Also Bought