Utumishi Unaotimiza Mapenzi ya Mungu
Changamoto si kumtumikia Mungu, ila ni kuyatimiza mapenzi ya Mungu kwenye utumishi ambao Mungu anakuwa amekuitia kutumika.
Kuingia kwenye utumishi ni kuitikia wito na kuyapokea majukumu ambayo Mungu anakupatia. Kumbe basi, mwamini yeyote anayesema hana utumishi, inakuwa si kwamba hana utumishi ila hajataka kuyapokea majukumu (kuitikia wito) kutoka kwa Mungu.
Tunapoingia kwenye utumishi yako mambo mengi tunayokutana nayo, mengine yanatutia nguvu na hamasa ya kuendelea mbele, na mengine yanatuvunja moyo kiasi cha kutaka kuacha utumishi wetu. Kabla hujafikiria kuacha utumishi, mwangalie Yesu kwanza alifanya nini kwenye utumishi wake, na ndani ya kitabu hiki tutajifunza mambo mengi kwa kumwangalia Yesu. Tutakubaliana kwamba Yesu ndiye kielelezo chetu kwenye mambo yote yahusuyo utumishi.
Kwa maneno haya machache, nikukaribishe sasa kusoma kitabu hiki. Ni maombi yangu kitabu hiki kiyaathiri maisha yako kwenye eneo la utumishi – furahia kumtumikia Mungu!
Amen
Recommended for you
Customer reviews
★★★★★
JAMES, 19 Sep, 2024
Yes, the service is very fantastic. When you purchase, instantly you get your copy. DL bookstore is a good website for every reader who needs good books.